Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 282
- 275
Matumizi ndio yanayotengeneza sura ama picha nzima ya kipato chako siku zote watu wengi wanafeli sheria ndogo ndogo kama hii ya matumizi ya pesa,hakikisha matumizi yako hayazidi kipato chako.
watu wengi wanatengeneza matumizi hadi yanapitiliza kiwango cha kipato chao na mwisho wake huishia kusema wanapata pesa lakini haionekani hiyo ni kwa sababu matumizi ya pesa yako juu hata kama ni mshahara umeshaumaliza kabla hata haujafika yaani ukipokea tayari wote unaishia kwenye madeni ya mwezi uliopita, ukijiona uko kwenye hali hiyo basi ni suala la msingi kuanza kuangalia kwa umakini matumizi yako ya mwezi,wiki ama siku ili utengeneze matumizi yenye uhalisia na yaliyondani ya kipato chako.
Ukiweza kusimamia matumizi yako yakawa chini ya kipato chako unakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya vitu vingine vya kukuongezea kipato hata kuweka akiba inayokaa.
#Maishanihayahaya siku inamasaa yale yale 24 kwa watu wote kinachotofautisha ni matumizi ya hayo masaa kwa mtu na mtu,jitathmini kama kuna cha kubadilisha badilisha bado #wakubadilikaniwewe
uwe na Jumatatu njema...