Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Ella Harper alizaliwa Januari 5, 1870 akiwa na tatizo la mifupa ambalo lilisababisha magoti yake kujipinda kwa nyuma hali iliyomlazimisha kutembea kama mnyama.
Ugonjwa wa mifupa aliokuwa nao ulikuwa unafahamika kama Congenital genu recurvatum. Ambapo kwa hali hiyo ilimfanya wamuite jina ‘The camel Girl’ au msichana ngamia.
Mwaka 1886 alijiunga na kikundi cha maonesho mbali na ulemavu wake na alikuwa akijipatia $200 kwa mwezi kama mshahara hali iliyoleta nuru katika maisha yake.
Harper alifariki Desemba 19, 1921. Hii inanesha walioendelea hawakuwa wanawafungia walemavu tangu enzi hizo, tofauti na nchi zinazoendelea ambapo mara nyingi watoto walemavu wamekuwa wakifichwa.