Nashauri sana walemavu wetu wasiachwe wawe ombaomba na kutumika kama kitega-uchumi (chuma ulete) kwa wenye uchu wa fedha. Hawa wanapaswa kutafutiwa kazi inayoendendana na hali zao, ili wajipatie kipato na kufurahia kuendesha maisha yao kama wengine. Hawakulemaa akili, bali sehemu tu za mwili wao.