Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Sasa imekuwa rasmi kuwa Ellon Musk ameyakataa maombi ya Ukraine kutumia mifumo yake ya mawasiliano katika eneo la Crimea.
Ellon amesema akiruhusu hilo itakuwa kama ameruhusu Urusi kutumia silaha za nyuklia.
Kwa upande wa maeneo mengine ya Ukraine amesema hawezi kutoa maelezo zaidi kwani ni siri za vita.
Amekanusha kuwa na mazungumzo na raisi Putin kuhusiana na uamuzi wake huo.
Pamoja na hivyo amethibitisha kukatikatika kwa mawasilano ya mifumo yake kwenye mistari ya mbele ya vita vinavyoendelea ikihisiwa Urusi wameanza kupata namna ya kuchafua mawasilano hayo ambayo katika siku za karibuni yameiwezesha Ukraine kusonga mbele kwenye uwanja wa vita.
Vifaa vyake hivyo ambavyo vinatumia nishati ndogo mwanzoni viliidhinishwa naye na serikala ya Marekani kama kuipa namna Ukraine kuingia maeneo yaliyokuwa mfu kwao kiteknolojia ya mawasilano.