SI KWELI Elon Musk alidhamiria kutorejesha akaunti ya Twitter ya Donald Trump kwa kuwa anamchukia

SI KWELI Elon Musk alidhamiria kutorejesha akaunti ya Twitter ya Donald Trump kwa kuwa anamchukia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Musk Trump Twitter Fake.jpg
UVUMI
Hivi karibuni baada ya Elon Musk kuununua mtandao wa Twitter kuliibuka uvumi kwamba bilionea huyo amepanga kurejesha akaunti zote za Twitter zilizofungiwa, kasoro ile ya aliyekuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021, Donald Trump.

Kichwa cha habari cha taarifa hiyo kinasomeka kwa Kiingereza: “Elon Musk States Intention to Restore Every Banned Twitter Account, ‘Except For Donald Trump’, huku ikifuatiwa na maandishi yasomekayo kwa Kiingereza: "It may seem petty but I just don’t like him"- ikimaanisha kuwa ni jambo linaweza kuoneka dogo, ila yeye (Elon Musk) hampendi tu Donald Trump.

Picha (screenshot) hiyo inayodaiwa kutoka ukurasa wa gazeti maarufu la Marekani, New York Times, imekuwa ikizunguka kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya Musk kuununua mtandao wa Twitter.

Hata hivyo, ni kweli kwamba akaunti ya Twitter ya Donald Trump iliyokuwa na wafuasi zaidi ya milioni 80 ilifungiwa mnamo 8 Januari 2021 kwa kuchapisha tweets ambazo zilienda "kinyume na sera za Twitter."

UKWELI NI UPI?
 
Tunachokijua
Picha hiyo inaonekana kuwa imetengenezwa kidigitali kwani kichwa cha habari kinachodai kuwa Musk kutokuwa tayari kuifungua akaunti ya Twitter ya Trump hakipatikani katika tovuti ya The New York Times au akaunti zake za mitandao ya kijamii zilizothibitishwa. Lakini pia, hakuna yeyote kati ya Trump au Musk ambaye amezungumza hadharani juu ya madai hayo.

Hata hivyo, tukirudi nyuma kidogo, mnamo mwezi Mei mwaka huu, Musk alieleza kuwa kitendo cha mtandao wa Twitter kumfungia Bw. Trump kwenye mtandao huo ilikua ni makosa makubwa na akaahidi akikamilisha mchakato wa kuinunua Twitter atamfungulia Trump.

Baada ya Musk kufanikiwa kuinunua Twitter mwishoni mwa Oktoba mwaka huu, mwezi Novemba aliweka chaguo la kura kuwataka watumiaji wa mtandao huo kuamua Trump arudi au asirudi.

Ndani ya saa 24 jumla ya Kura zilizopigwa zilikuwa ni 15,085,458, na baada watu milioni 7.8 wataka Trump arudi Twitter, Elon alikubali kumrejesha. Akaunti ya Twitter ya Donald Trump sasa imefunguliwa na inaweza kuonekana hapa.

Hivyo basi, taarifa ya kuwa bilionea Musk alipanga kutorejesha akaunti ya Twitter ya Donald Trump ilikuwa ni uzushi tu.
Back
Top Bottom