Elon Musk ana gundu gani na Tanzania?

Elon Musk ana gundu gani na Tanzania?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wiki imeanza kwa raia wenzetu mbalimbali katika hii nchi kwenye nafasi za kisiasa za chama tawala na wale wa upande kidini kuitaka serikali ifungie mtandao wa Twitter/X

Pia itakumbukwa Starlink kampuni ya mtandao ya Elon Musk imeshindwa kupata kibali cha kufanya kazi Tanzania ikesemwa na Nape kwamba wameshindwa kukidhi vigezo vya kupata kibali.

Nafikiri pia hakuna hata gari moja la Tesla bongo, pia PayPal kampuni yake nyingine aliyowahi kuwa muwekezaji wake nayo nasikia haiwezi kufanya kazi zake kiutimilifu Tanzania.

Huyu tajiri namba moja machachari sana ni kama ana gundu na Tanzania. Hii inaweza pia kuwa fursa kwa wabongo watakaoweza kumnyooshea mambo yake nchini.
 
Back
Top Bottom