Unamaanisha hajui kabisa pesa zake zinawekezwa wapi,siyo!?Unajua kampuni inavyoendeshwa wakati wa ishu za mazungumzo ulimuona Elon kwenye picha, Meta walivyotembea TZ ulimuona Zuck kwenye picha.
Wanao negotiate na ku-push kilakitu ni watu watching ya Musk yeye katulia tu.
Tunajipa umuhimu ambao hatunao wakati hatuna kila kitu.Ukweli mchungu ni kuwa hatumuongezei wala kumpunguzia chochote na ujinga wetu
Ni juzi tu ndio wameruhusu gari za umeme kuja bongo. Zilikuwa hazijaruhusiwa na serekali ya fisiemu. Kuna uzi humu unazungumzia mambo hayo na ukiritimba uliokuwepoHata Mtumba wa Tesla hauko Bongo kweli?!
Mchango wa Tanzania kwenye biashara za Musk ni kidogo sana, hivyo Tz sio tishio kwenye biashara zake. Kwenye huduma ya internet ya stalink, nadhani hapa Serikali iliangalia kodi na shares zake kwenye makampuni ya simu kuliko kujali mzigo wa gharama kwa watumiaji. Stalink ikianza kufanya kazi hapa, vodacom, airtel na nyinginezo zinakufa. Huenda hata haya makampuni ya simu yanapambana kwa NJIA zote ili Musk apigwe chini.Wiki imeanza kwa raia wenzetu mbalimbali katika hii nchi kwenye nafasi za kisiasa za chama tawala na wale wa upande kidini kuitaka serikali ifungie mtandao wa Twitter/X
Pia itakumbukwa Starlink kampuni ya mtandao ya Elon Musk imeshindwa kupata kibali cha kufanya kazi Tanzania ikesemwa na Nape kwamba wameshindwa kukidhi vigezo vya kupata kibali.
Nafikiri pia hakuna hata gari moja la Tesla bongo, pia PayPal kampuni yake nyingine aliyowahi kuwa muwekezaji wake nayo nasikia haiwezi kufanya kazi zake kiutimilifu Tanzania.
Huyu tajiri namba moja machachari sana ni kama ana gundu na Tanzania. Hii inaweza pia kuwa fursa kwa wabongo watakaoweza kumnyooshea mambo yake nchini