incognitoTz
Senior Member
- Apr 19, 2019
- 133
- 172
Elon Musk anataka SpaceX kuongeza majaribio ya kurusha roketi ya Starship kutoka mala 5, 2024 hadi 25 kwa mwaka 2025. Hata hivyo mpango huo wa kuongeza hiyo idadi unahitaji idhini ya FAA.FAA, Federal Aviation Administration ndio yenye mamlaka ya kutoa vibali vya kurusha roketi za kibiashara.
Starship ni roketi kubwa inayoweza kutumika tena (re-usable), iliyoundwa kwaajili ya safari za Mwezini na Mars. Kumekuwa na wasiwasi juu ya athari za kimazingira na kukidhi kwa vigezo vya kufanya ongezeko hilo.
Musk amekuwa na mikwaruzano ya mala kwa mala na FAA juu suala hilo, huku akiishutumu mamlaka hiyo juu ya unyanyasaji wa kiudhibiti. Hali inayoweza kubadirika kipindi hiki ambacho Elon Musk anaendakuwa sehemu serikali ya Marekani katika idara ya uwajibikaji na ufanisi huku rafiki yake wa karibu Jared Isacman akitarajiwa kuapishwa kuwa mkuu wa NASA Januari 20, 2025.
Licha ya ongezeka la idadi ya majaribio ya Starship kuwa na tija katika maendeleo uchunguzi wa anga bado vikwazo vya kimazingira na kiudhibiti vinaweza vikazuia jitihada hizo.