Elon Musk kuimiliki twitter 100%

Elon Musk kuimiliki twitter 100%

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Mtu tajiri zaidi juu ya uso wa Dunia kwa paper assets mzaliwa wa Africa mwenye uraia wa Marekani ametangaza kuwa tayari kuinunua kampuni ya twitter kwa gharama ya $54 kwa kila hisa.

Ikumbukwe mpaka sasa Elon ambae yuko active sana kwenye mtandao wa twitter anamiliki 9.2% ya hisa za twitter akimzidi mpaka mwanzilishi wa mtandao huo mmarekani Jack Dorsey.
 
Elon Musk huwa anaona mbali sana, hiyo hela atakayolipa inaonekana ndefu lakini yeye kisha ipigia mahesabu na kuona kuwa itarudi upesi sana mara atakapoimiliki hiyo TWITTER!!!
mpaka dakika hii keshakunja 38% ya pesa yote aliyonunulia hisa za twitter
 
mpaka dakika hii keshakunja 38% ya pesa yote aliyonunulia hisa za twitter
Duh bila shaka kwa tamko lake hili thamani ya hisa itapanda.
Niliona anachunguzwa yeye na ndugu yake kwa kumanipulate hisa za tesla kisha kuuza wanasema matamshi yake aliyotoa kabla ya kuuza hisa huenda ni makosa.
 
Duh bila shaka kwa tamko lake hili thamani ya hisa itapanda.
Niliona anachunguzwa yeye na ndugu yake kwa kumanipulate hisa za tesla kisha kuuza wanasema matamshi yake aliyotoa kabla ya kuuza hisa huenda ni makosa.
Ameshashtakiwa tayari na baadhi ya wenye Hisa wa twitter.

Amenunua Hisa kisiri siri then hajasema na hapo anatia watu sound ili hisa zipande, hisa zikipanda ujue yeye ndio ananufaika kwa hisa za Awali.
 
Atawalipa SEC fine kidogo na ataendelea na manipulation zake huyu tajiri wa mchongo
Unajua mimi uwa napenda sana tazama channel za youtube za mbele huko na kusoma comments uwa napenda sana comments. Sasa niliona wazungu wanamsema kuwa jamaa mtu wa manipulation sana si ndo nikajua kuwa hata tesla hakuoanzisha yeye kama watu wanavyoamini.
Sema he is smart. Kama kuna jambo liliwahi nivutia ni jinsi zile rocket zake zilinavyoenda space kisha zikarudi na kutua vertically. Nakumbuka ile alipolaunch lile gari la tesla rocket zilivyotua alikuwa so excited ile kitu inafurahisha sana
 
What type of censorship do you experience when you use TWITTER? Is it the absence of the "EDIT" button?
Hili swali akiulizwa Donald Trump au yule mtoto wa Museveni au Rais wa Nigeria - Buhari watakujibu vizuri.
 
Back
Top Bottom