Elon Musk: Twitter kumfungia Trump maisha haikuwa sahihi, aahidi kurejesha Akaunti ya Twitter ya Trump

Elon Musk: Twitter kumfungia Trump maisha haikuwa sahihi, aahidi kurejesha Akaunti ya Twitter ya Trump

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Bilionea Musk amesema kitendo cha mtandao wa Twitter kumfungia maisha aliekua rais wa Marekani Bw. Trump kwenye mtandao huo ilikua ni makosa makubwa na ameahidi akikamilisha mchakato wa kuinunua Twitter anamfungilia Trump.

Bw. Musk yeye anajiita muumini mkubwa wa uhuru wa kujieleza usio na mipaka ama free speech absolutionist isipokua mipaka hiyo imewekwa na sheria ila sio wahuni tu wachache kuamua kumfungia mtu kwa kua hawapendi maoni yake.

Mwezi uliopita Trump alisema anajua Musk ni mtu mwema ila yeye alisema hatarudi Twitter badala yake ataendelea na mtandao wake wa Truth Social.

Binafsi nitafurahi kumuona tena Bw. Trump Twitter. Sikukubaliana kabisa na Twitter kumfungia Trump.

Elon amekuja kutuokoa kutoka kwenye mikono ya magenge ya wahuni wasiopenda mawazo ya wenzao.
 
Don hana mpango nayo tena yupo busy na truth app yake haha
 
Back
Top Bottom