Em Naombeni Mwongozo Wenu JF Great Thinkers ...!


Nadhani hapa tatizo sio wewe, mkeo wala mwanenu. Tatizo ni hiyo shule anayosoma. Ongea na walimu waamue kuwapa watoto commom breakfast (uji and snack or uji pekee) au wasitoe kabisa breakfast hapo shule na kila mzazi amfungashie mwanae snack.

Kumpa mtoto mia mbili, au hata mia tano au hata elfu ni kukubaliana na ukware wa hao walimu kuamua kuwalisha watoto wenu chochote wawapo shuleni bila consent yenu.
 

Mie sioni kama ni tabia mbaya, nakumbuka wakati nasoma nilikuwa nikipewa shilingi 25 kila siku pamoja na nauli ya dala dala na hizi zilikuwa nyingi hata ukitaka kujichana zilikuwa zinatosheleza kabisa na weekend bado ukabaki na pesa za kwenda movie ila kama kwenda kuruka majoka basi ilikuwa inabidi upige bomu lingine ili ukaruke majoka. Kama uwezo unakuruhusu basi ongeza hado 500, 200 kwa sasa ni pesa ndogo sana kwa siku.
 
Hamna ubaya wowote kumpatia mwanao pocket money ila usizidishe sana kiwango yaani badala ya kumpa ile inayomtosheleza kwa siku (kama shilingi 200/=) ukampa elfu kumi hela ya kutumia shuleni kwa siku moja hapo utakuwa unamharibu mwanao. Ipo siku utakuwa huna na mtoto akagoma kwena shule na pia waweza kumfungashia chakula toka hapo nyumbani.
 
Wakati mwengine wanawake wanakuwa wakali kwa watoto wa kike kwa mambo ya kawaida kabisa.
Kama uko vizuri, mpatie 500/= daily.
Mkuu 500.- is on a high side,mimi nashauri mtoto apewe sh 300.- ambayo inatosha kununua mandazi mawili mazuri ya bakhresa.Mtoto hapashwi kuwa starved si sawa,apewe mia tatu na mama aache unoko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…