Emanuel Mbasha: Shilole pambana na hali yako, usipende mteremko

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha ameamua kuwatolea uvivu Shilole akimtaka aache kupenda vya dezo apambane na hali yake.

Wiki mbili zilizopita Shilole alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari chini akiomba msaada kwa Rais Magufuli wa kumsomesha mtoto wake mmoja wa kike ambae amedai kuwa baba yake mzazi amefariki dunia.

Mbasha ameshangaa msanii mkubwa kama Shilole kuhitaji msaada wa ada ya kumsomesha mtoto wake ile hali anafanya kazi na ni mjasiriamali huku majuzi amejisifia kujenga nyumba za zaidi ya milioni 90.

Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya Raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie. Jamani sera ya Raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema “HAPA KAZI TU” Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kuku cost 😁😁😁😁.

Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili😭.😭😭😭.

Leo nimeshangaa kuona clip inasambaa ukilia na kuomba Rais akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri.

Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je ! Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ?

Je ! Huyo unaetaka asomeshwe yuko darasa la ngapi dada yangu?
Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua.
Hebu jiulize, leo Rais akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama ??,
“ameandika Emmanuel Mbasha kwenye ukurasa wa Instagram na kutoa ushauri kwa Shilole.


Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko. Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa ?

Mimi nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa rais, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.

Mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea rais na ukaomba akudhamini ili upate pesa Bank 400 Ml au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo,

Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angalau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye.

Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani.
Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kula.
Kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima. kajifunze kwa @munalove100 basi,
“ameeleza Mbasha.

Kwa upande mwingine Shilole amemjibu kwa kusema
Nakuheshimu sana kaka yangu, please tulinde heshima yetu”.

Wiki mbili zilizopita Shilole alikaririwa kwenye vyombo vya habari akiomba msaada kwa Rais Magufuli wa kumsomesha mtoto wake mmoja wa kike ambae amedai kuwa baba yake mzazi amefariki dunia.

Source: Bongo 5
 
Mbasha yuko sahihi kabisaaa. Wasanii wa bongo wanatudhalilisha sana sio siri. Sijaona msanii wa Tanzania aliye tulia zaidi ya upuuzi tu.. sasa shishi jamani anataka msaada upi wakata ana biashara zake jamani..
 
shilole anashindwaje kuhudumia akati alisema ye ni msanii mkubwa na tajiri kwa upande wa KE
 
Huyu jamaa hayupo sawa kisaikolojia naona anahangaika sana kushinda mwanamke wake wa zamani frola mbasha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…