ASKOFU ATAJA USHAHIDI WA KI-BIBLIA WA KWANINI WAKRISTO HUABUDU JUMAPILI!
Kwa mujibu wa Biblia, siku ya saba ya juma ni Jumamosi, siku ya kwanza ya juma ni Jumapili. Tangu mwanzo, Wayahudi walikuwa na dini yao (Judaism) ambayo hadi leo ipo na ndio dini kuu nchini Israel. Dini nyingine katika nchi ya Israeli ni Ukristo na Uislamu.
Katika miaka ya mwanzo wa Ukristo, watawala wa Kirumi walifikiri kuwaUkristo ni dhehebu au tawi mojawapo katika dini ya hiyo ya Kiyahudi. Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyopekea, Warumi wauvumilie Ukristo hapo mwanzoni kwa kuwa Warumi hawakutaka kijiingiza katika mogogoro ya dini ya Kiyahudi (Matendo 23:13-30). Lakini, walipogundua kuwa Ukristo haukuwa sehmu ya dini ya Kiyahudi, walianza kutesa Wakristo. Hivyo basi, Wakristo walikuwa wanateswa na Warumi na waliteswa na Wayahudi pia.
Jumamosi ilikuwa ndiyo siku maalum ya ibada kwa mujibu wa dini ya Kiyahudi na ndio maana siku ya Ijumaa Kuu waliamua kuuzika mwili wa Yesu mapema ili kuepuka kufika siku ya ibada ambayo ilikuwa inaanza saa 12:00 Ijumaa jioni.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizohifadhiwa katika maandiko matakatifu (Biblia), kusanyiko la kwanza kufanywa na wanafunzi (mitume) wa Yesu baada ya la Jumatano kabla ya Alhamisi Kuu; ilikuwa siku ya kwanza ya juma (Jumapili), siku aliyofufuka Yesu. Baadaye, wanafunzi wa Yesu waliendelea kukutana siku hiyo kumega mkate kama ilivyokuwa desturi.
Hata hivyo, mitume waliendelea kwenda katika masinagogi kufundisha wakiamini kuwa hata Wayahudi wengine watamuamini Yesu kuwa ni masihi. Lakini Kitendo cha mitume hao kwenda kufundisha katika masinagogi, kilizua vurugu na mitafaruku sana. Mashtaka dhidi ya Mtume Paulo yaliyoandikwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume ni ushahidi wa jambo hili.
Ikumbukwe kuwa, Ukristo ulopokuwa unaanza kama dini, hakukuwa na maelekezo kuhusu juu ya siku ya kusali. Kwanza kabisa, Wakristo wa kwanza waliamini kuwa Yesu angelirudi mara moja, hivyo hawakuwa na muda wa kupoteza kuhusu kujadiliana juu ya mambo ya dini na pia mifumo yake ikiwemo siku maalum ya ibada. Ushahidi kuhusu hili unapatikana katika kitabu cha 1 & 2 Wathesalonike.
Kwa hiyo, Wakristo wa kwanza hawakujali sana kuwa na siku maalum ya kusali na hawakuwa na majengo maalum ya kufanyia ibada. Ingawa kila siku ya Jumapili waliendelea kukusanyikia katika nyumba za waumini au viongozi wao ili kumega mkate na kusali. Kitendo cha kumega mkate na kusali kila walipokutana huitwa Misa. Hii ndio sababu hadi leo baadhi ya Makanisa hushiriki Ushirika Mtakatifu kila siku ya ibada.
Sababu za Wakristo wa kwanza kuabudu siku ya kwanza ya juma (Jumapili) ni hizi zifuatazo:
1. Jumapili Ilikuwa ni Siku ya Kufufuka kwa Yesu, kwa hiyo waliendelea kukusanyika kwa ajili ya kumega mkate na kutiana moyo.
2. Wakristo hawakutaka kufungwa na siku au mapokeo ya sheria za Kiyahudi kwani walijiona kuwa wako juu ya mapokeo. Rejea uamuzi wa mkutano mkuu wa kwanza wa Kanisa ambao uliitishwa na Mtume Yakobo mwaka 44 (BK) kule Yerusalemu (Matendo ya Mitume 15:1-35).
3. Justin anasema kuwa Sunday ilikuwa ni Sun Day (Siku ya Jua), ambayo ilihusiana na ibada za uumbaji. Hivyo ilikuwa rahisi kuhusianisha na dhana ya Ukristo kwa sababu Kristo alitajwa kama Jua la Haki (Malaki 2:4) na pia alitajwa kuwa ni 'Nuru ya Ulimwengu (Yohana 9:5).
4. Justin pia anasema kuwa Jumapili ilikuwa ndio siku ya kwanza ya uumbaji, Mungu aliposema na 'iwe nuru'.
5. Katika maandiko ya Agano Jipya, Jumapili ilianza kuchukua nafasi ya Jumapili kama siku ya ibada kwa Wakristo (Matendo 20:7; 1 Wakorintho 16:2.
6. Mtume Yohana anaitaja Jumapili kama ndiyo Siku ya Bwana (Ufunuo wa Yohana 1:10).
Tunaandika kusudi kuwajenga kiimani Wakristo wanaoyumbishwa na mafundisho yanayokaza siku za ibada kama ndio msingi wa imani yetu. Kwa ujumla, Wakristo wanaweza kukutana siku ye yote na kufanya misa au ibada bila kubanwa na mapokeo ya siku kutegemea na mazingira.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, ambaye ni mwandishi wa makala hii, ni mhadhiri wa falsafa, theologia, ecclesiologia (historia ya Kanisa), literature, soshologia na utafiti. Amefundisha masomo hayo kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu, St. John's University of Tanzania.
Dar es Salaam, 1 Aprili 2024; saa 14:45 alasiri