Embu nishaurini

Za jioni natumai wote mmekula na kushiba!

Mwezenu sasa hapa nimepata ka feeling fulani hivi yaani natamani mtoto wa mtu anipende two yaani anione wivu mda wote yaani mda wote aniembie tu ilove you

Natamani nimpendeeeeee sna mda wote niwe nae karibu
Muda si mcahche utageuka bawna Alinacha. Alinacha alipiga teke kapu la vikokoro vyake baada ya kuwaza kuwa amefanya biashara ya umachinga akawa tajiri, akaoa binti mzuri sana, akawa anamfanyia maringo huku mama yake binti akimbembeleza anyooshe walau mkono wake amshike binti mwisho akarusha teke na umachinga ukaishia hapo hapo.
 

Mbona kma unachana
 
[emoji23][emoji23][emoji23] najua hilo
Hapo kale paliondokea mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili ambaye mmoja wapo kati kati ya hao aloiitwa Al – Nacha na nduguye, ambao mara baada ya baba yao kufa kwa ajili ya uzee aliwaachia kila mmoja kiasi cha fedha reale 100.
Ama kwa hakika fedha hizo zilikuwa ni nyingi sana kwa wakati huo, na Al – Nacha alipoona kuwa fedha ni nyingi kiasi kile hakujua hata namna ya kuzitumia.
Walakini baada ya kufikiri kidogo akakata shauri kufanya biashara ya kununua na kuuza vyombo vya glasi. Siku moja alikwenda akanunua bidhaa za reale 100 ambacho ni kiasi chote alichokuwa nacho, na baada ya kuzitia katika kapu kubwa akaenda nazo kwenye pembe ya ukuta mmoja mkubwa wa barabara moja kuu iliyokuwa ikipitiwa na watu wengi.
Ijumaa moja wakati alipokuwa amekaa pale na bidhaa zake alianza kuwaza, “Raslimali yangu yote nimeitia katika bidhaa hii ya glasi tupu bila shaka nitaiuza kwa bei ya reale 200.
“Kwa fedha hizo nitakazozipata nitanunulia tena bidhaa zingine za aina hii ambazo nazo nitaziuza kwa reale 400, nitaendelea kufanya hivyo mpaka nitakapopata utajiri mkubwa sana wa kuniwezesha kuanzisha mtaji mkubwa wa biashara ya almasi, lulu na mawe mengine ya tunu.
“Kwa utajiri nitakaoupata nitanunulia kila aina ya vitu vya tunu na anasa na kisha kuviuza, kwa faida kubwa niutakayoipata nitanunua nyumba kubwa ya kifahari iliyojaa wajakazi watakaoningojea mbele ya nyumba yangu huku wakishikilia farasi wangu aliye na hatamu za dhahabu na tandiko la zari la thamani kubwa.
“Kila siku nitakula vyakula vya namna namna vilivyotayarishwa kwa mapishi ya hali ya juu na nitakunywa divai ghali sana inayopatikana kwa nadra wakati huku nikitumbuizwa nyumbani kwangu na waghani mashuhuri wenye sauti za ajabu watokao sehemu mbalimbali za nchi za jirani.
“Baada ya muda, waghani wote mashuhuri wa kike na wa kiume nchini watafika mara kwa mara kwangu kunitumbuiza na kunistarehesha.
“Baada ya muda si mrefu, fedha zangu zitatimia lukuki, na hapo nitawaajiri watu mashuhuri waende wakanitafutie msichana mzuri kutoka katika mabinti wa Wafalme na mabinti wa Mawaziri mashuhuri nkwa ajili ya kumuoa.
“Labda nitamposa binti wa Waziri Mkuu kwani nasikia kuwa uzuri wake hauna kifani! Ile kupeleka tu mjumbe wa kuniposea nitamtunukia Waziri Mkuu zawadi ya fahari ya thamani ya reale elfu moja za dhahabu safi asli. Na kama ataonesha kusitasita au atakataa, nitamchukua binti wake kwa nguvu! Kisha nitamnunulia binti huyo wajakazi kumi vijana wa kumhudumia na kumsimamia; mimi mwenyewe nitajipamba kwa lebasi ghali za fahari na vito vya tunu.
“Wakati nitakapompanda farasi wangu na kupita njiani kuelekea kwa Waziri Mkuu, huku mbele nikiongozwa na watumwa wangu na nyuma nikiandamwa na watumishi wangu, watu watakuwa wakiniinamia kwa heshima na kuniamkia kwa unyenyekevu na kuniombea dua na kunisifu.
“Nitakapoingia katika Kasri ya Waziri, atanyanyuka na kunipokea kwa heshima kisha atanipisha nikikalie kiti chake na yeye mwenyewe atakaa chini ya miguu yangu.
“Hapo wawili wa watumwa wangu watamwekea miguuni pake mifuko miwili ambayo kila mmoja umejaa reale elfu moja za dhahabu.
“Mmoja nitampa kama mahari ya binti yake na wa pili utakuwa ni zawadi ya kumthibitishia umuhimu wa thamani yangu lakini nitakuwa kimya! Na kwa kila maneno kumi atakayoniambia, mimi nitamjibu kwa maneno mawili tena ya mkato. Halafu nitarejea kwangu.
“Wakati kila mmoja wa jamaa ya mke wangu atakaponitembelea, nitamnunulia joho la heshima la gharama kubwa na nitampa pia zawadi za dhahabu. Akiniletea zawadi yoyote, mimi nitairudisha ilikotoka ili ajue jinsi nilivyokuwa na kiburi pamoja na majivuno!
“Mimi mwenyewe nitachagua siku ya kufanya harusi yangu, na gaharama zote za sherehe zitakuwa ni juu yangu.
“Usiku wa harusi nitavalia joho moja kati ya yale majoho yangu ya thamani kubwa huku nikizungukwa na wageni walioalikwa rasmi kuhudhuria tafrija hiyo niliyoiandaa.
“Wakati wote huo nitakuwa nimeegemea mito mikubwa minene inayonakshiwa kwa nyuzi za zari na hariri. Sitageuka kushoto wala kulia, ila kwa maringo makubwa, nitatazama mbele tu.
“Bibi harusi atakapoletwa mbele yangu akiwa amevalishwa nguo za hariri na amepambwa kwa vito vya tunu huku amefunikwa gubigubi kwa ushungi wa hariri, sitamwangalia hata! Wasichana watakaomsindikiza watanisihi wakisema:
“Seyyid yetu, mbele yako kasimama mkeo mtumwa wako anayesubiri umfanyie hisani ya kumtupia jicho la huruma.”
“Wakati wakisema hivyo wasichana hao watajibwaga mbele ya miguu yangu na kunipigia magoti wakiibusu sakafu. Hapo nitamtupia mke wangu jicho la dharau na kuendelea kutazama kwingine, halafu watamwongoza mpaka katika chumba cha kulala.
“Baada ya muda nitanyanyuka kwenda kubadili nguo zangu kwa kuvaa joho jingine laini la tahamani, hapo nitamwamuru mmoja wa watumwa wangu aende akaniletee sarafu mia tano za dhahabu ambazo nitawamwagia wale waliomsimamia mke wangu kisha nitaingia kwa maringo chumbani kwa mke wangu.
“Nitakapokuwa naye peke yangu nitamwangalia tu wala sitamsemesha. Hapo mamiye ataingia ndani, na kisha atalibusu paji la uso wangu akisema kwa unyenyekevu:
“Seyyid yangu, nakusihi mtazame mjakazi wako anakusubiri kwa hamu. Mwonee huruma kwa kusema naye japokuwa neno moja ili uutibu moyo wake uliojaa huzuni.”
“Sitamjibu. Hapo atajiangusha chini na kuanza kuibusu miguu yangu akisema: “Seyyidina wangu, mjakazi wako si mzuri tu wa sura bali ni mwanamwali ambaye bado hajaonana na mwanamume yeyote. Tafadhali niko miguuni pako; nakusihi usimnyamazie na kumtesa hivyo ama sivyo atakuwa na majonzi mengi.”
“Hapo mama mkwe wangu atanyanyuka, atanimiminia divai katika bilauri kisha atamkabidhi binti yake aniletee. Binti Waziri atapiga magoti mbele yangu na kunipa hiyo bilauri, lakini mimi ambaye wakati huo wote nimekaa na kuegemea mito mizuri minene iliyonakshiwa sitamwangalia wala kumjali.
“Kwa sauti ya unyenyekevu na ya kutetemeka mke wangu atasema: “Seyyid yangu, nakusihi pokea bilauri hii kutoka mikononi mwa mtumwa wako.”
“Lakini sitamjali bali nitatazama kwingine na kubaki kimya! Baada ya muda ataielekeza ile bilauri mdomoni kwangu akiendelea kunisihi niinywe. Lakini nitausumkuma mkono wake na kumpiga teke la nguvu!”
Hapo Al – Nacha alipokuwa kisema hivi bila kujijua akalipiga lile kapu kubwa lililokuwa na vyombo vya glasi vyenye thamani kubwa, lililojaa bidhaa lukuki na kuvunjilia mbali kila kilichokuwamo mle ndani!
Kumbe yote hayo yalikuwa ni mawazo tu na wala hakuuza hata chombo kimoja! Na kwa kuwa kila alichokuwa nacho mle kapuni kilivunjika tikitiki, na kwa kuwa tayari alikwishatumia reale zote ambazo ndizo zilikuwa ni ngama yake; akarudi kuwa maskini zaidi ya alivyokuwa.
 

Sasa rafiki yangu hii insha nitaweza kuisoma kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…