Hili tatizo la waamuzi Tanzania nilidhani ni makosa ya kibinadamu kumbe ni makusudi.
Leo kuna kihoja kimetokea mechi ya Dodoma Jiji Vs Mtibwa uwanja wa Liti Singida. Dakika ya 82 mchezaji wa Dodoma Jiji Emmanuel Martine alifanyiwa madhambi nje ya eneo la 18 lakini akaendelea kwenda hatua 3 akaingia eneo la 18 na kuanguka.
Emmanuel Mwandembwa akaweka Penati. Kumfungia Arajiga na kumwacha Mwandembwa hata kama Dodoma Jiji wamekosa hiyo penati ni kuunga mkono uhuni wa hawa wanaojiita Waamuzi Wasomi.