KWELI Emmanuel Nwude wa Nigeria aliwahi kuuza Uwanja wa Ndege 'usiokuwepo' kwa Dola Milioni 242

KWELI Emmanuel Nwude wa Nigeria aliwahi kuuza Uwanja wa Ndege 'usiokuwepo' kwa Dola Milioni 242

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1729146706043.png
Inasemekana kuwa Emmanuel Nwude, mmoja wa matapeli maarufu zaidi katika historia ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria ambaye kati ya miaka ya 1995 na 1998, aliwahi kumuuzia mtu uwanja wa ndege wa bandia, akijifanya kuwa mkurugenzi wa Benki Kuu ya Nigeria.

Kwa udanganyifu huu, Nwude alimdanganya meneja wa benki ya kigeni huko Brazil, Nelson Sakaguchi, kuwa Nigeria ilikuwa ikijenga uwanja wa ndege wa kimataifa mpya huko Abuja, na kumshawishi kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa.

Kuna ukweli kiasi gani hapa?
 
Tunachokijua
Emmanuel Nwude ni raia wa Nigeria ambaye alikuwa ni miongoni mwa wafanyabiashara matajiri miaka ya 1990. Nwude alikuwa maarufu zaidi na taarifa zake kusambaa sana baada ya kushitakiwa kwa ulaghai alioufanya kwa benki ya Noroeste ya nchini Brazil.

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo kwa njia ya mtandao na taarifa mbalimbali zilizotolewa na tovuti za nchini Nigeria na maeneo mengine na kubaini kuwa taarifa hiyo ni ya kweli. Emmanuel Nwude ameelezewa kama miongoni mwa watu waliowahi kufanya utapeli mkubwa ulimwenguni.

Tovuti ya pulse inaeleza kuwa wakati anakamatwa kwa mara ya kwanza Emmanuel Nwude alikuwa ni miongoni mwa wafanyabiashara matajiri zaidi nchini Nigeria, Nwude anajulikana pia kwa jina la Owelle wa Abunug. Nwude alikamatwa kwa makosa ya kuuza uwanja wa ndege nchini Nigeria ambao haukuwepo kabisa.

Nwude alitumia utambulisho wa aliyekuwa Gavana wa benki kuu nchini Nigeria kuanzia mwaka 1993 hadi 1999 Paul Ogwuma, pamoja na nyaraka za kugushi ili kujipatia kiasi cha pesa cha Dolla milioni 242 kutoka katika benki ya Banco Noroeste Ya nchini Brazil.

Tovuti ya The guardian ya nchini Nigeria Nwude alimueleza msimamizi wa Benki ya Noroeste ya nchini Brazil, Mr Nelson Sakaguchi kuwa Nigeria wanahitaji muwekezaji wa uwanja wa ndege, Abuja na kiasi cha Dolla Milioni 242 kinahitajika na kama mpango huo utafanikiwa basi Sakaguchi atapata 10% kutoka katika kiasi hiko. Kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 1998, Sakaguchi alihamisha kiasi cha Dolla Milioni 191 taslimu kwa Nwude na washirika wake. Na nyingine ziliwasilishwa kama aina fulani ya riba.

Tovuti ya Bolagu Utapeli huo ulikuja kubainika mwaka 1997 kipindi ambacho benki ya Santander kutokea nchini Hispania Walihitaji kununua benki ya Noroeste na katika uchunguzi wao kuhusu thamani na kiwango cha fedha ya benki hiyo walibaini kuwa kiwango kikubwa cha fedha kipo nje ya benki hiyo katika maeneo tofauti ulimwenguni ikiwemo visiwa vya Cayman bila kufuatiliwa. Na hapo ndipo uchunguzi wa kina ukaanza. Kutokana na hali mbaya ya kifedha iliyokuwepo katika benki ya Banco Noroeste Wamiliki wa benki hiyo walilazimika kutoa pesa mifukoni mwao ili kufidia upotevu huo, lakini bado haikufaa kitu kwani mwaka 2001 Benki hiyo ilikufa.

Kwa mujibu wa pulse Mwaka 2003 Nwude alikamatwa akiwa nyumbani kwake huko Lagos na Kushtakiwa kwa makosa hayo ya ulaghai, ambapo washirika wake Amaka Anajemba, Nwude, Emmanuel Ofolue, Nzeribe Okoli, na Obum Osakwe, pamoja na Ikechukwu Anajemba nao mwaka 2024 walifikishwa mahakama ya shirikisho Abuja.

Tovuti ya ya nchini Nigeria wanaeleza kuwa Mwaka 2005, Emmanuel Nwude alifungwa kifungo cha miaka 25 kwa kusababisha kuanguka kwa benki katika nchi ya kigeni lakini pia kuleta masaibu kwa watu wengi wasio na hatia, lakini mwaka 2006 Nudwe aliachaliwa na kurudishiwa kiwango cha Dolla kwa kudai kuwa kiwango hikokilipatikana kabla ya tuhuma hizo.

Baada ya Nwude kuachiwa mwaka 2006 alifungua kesi ya kurejesha mali yake baada ya kuachiliwa kutoka gerezani. Akieleza kuwa baadhi ya mali zilipatikana kabla ya kutenda kosa hilo ambapo alifanikiwa kurudishiwa dola za Kimarekani milioni 52, inaeleza kuwa a tovuti ya medium.
Ni kweli, Emmanuel Nwude alihusishwa na alimdanganya Nelson Sakaguchi ambaye alikuwa meneja wa benki ya Banco Noroeste ya Brazil na kumfanya aamini kuwa ananunua uwanja wa ndege mpya nchini Nigeria.

Kati ya mwaka 1995 na 1998, Nwude alijifanya kuwa Paul Ogwuma, Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Nigeria, na alimdanganya Sakaguchi kuwa Nigeria ilikuwa ikijenga uwanja wa ndege wa kimataifa mpya huko Abuja. Alimshawishi Sakaguchi kuwekeza katika "mradi" huu na hatimaye kufanikiwa kumtapeli takriban dola milioni USD 242.

Umaarufu wa utapeli huu wa Nwude unatokana na ukubwa wa kiwango cha fedha kilichohusishwa na jinsi Nwude alivyoweza kumshawishi Sakaguchi bila kuwapo mradi halisi wa uwanja wa ndege. Jamaa alikamatwa mwaka 2004 na kufikishwa mahakamani ambapo alikutwa na hatia katika makosa mbalimbali yaliyomkabili na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha miaka mingi jela pamoja na kulipa fidiaa.

Zaidi soma hapa chini

 
Inasemekana kuwa Emmanuel Nwude, mmoja wa matapeli maarufu zaidi katika historia ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria ambaye kati ya miaka ya 1995 na 1998, aliwahi kumuuzia mtu uwanja wa ndege wa bandia, akijifanya kuwa mkurugenzi wa Benki Kuu ya Nigeria.

Kwa udanganyifu huu, Nwude alimdanganya meneja wa benki ya kigeni huko Brazil, Nelson Sakaguchi, kuwa Nigeria ilikuwa ikijenga uwanja wa ndege wa kimataifa mpya huko Abuja, na kumshawishi kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa.

Kuna ukweli kiasi gani hapa?
Kuna watu walishawahi kuuziwa mnara wa Paris maboya ni wengi sana hapa duniani.
 
Huyo ni tapeli wa manufaa.
Sasa wewe unamtapeli mstaafu wa Tanganyika ambaye kiinua mgogo chake kapewa 30% tena kwa masimango na michosho mingi.
 
Back
Top Bottom