Emmanuel Okwi aing'arisha 'The Cranes' aingia kambani mara mbili kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Lesotho

Emmanuel Okwi aing'arisha 'The Cranes' aingia kambani mara mbili kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Lesotho

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes' imejiimarisha kileleni kwenye kundi L katika michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019, nchi Cameroon baada ya kuichapa Lesotho mabao 3-0 kwenye uwanja wa Namboole mjini Kampala Uganda.

Uganda Cranes, wamefikisha alama saba baada ya mechi tatu, wakifuatiwa na Cape Verde yenye alama nne huku Tanzania na Lesotho wakiwa na alama mbili.

Ukurasa wa mabao ulifunguliwa na Emmanuel Okwi anayekipiga kunako timu ya Simba SC ya Tanzania katika dakika ya 11 kabla ya mchezaji Farouk Miya wa NHK ya Croatia kuandika bao dakika ya 36.

Ukurasa ulifungwa kama ulivyofunguliwa na yule yule Emmanuel Okwi kwa bao safi la kichwa katika dakika ya 63 ya mchezo.

Timu hizo zitarudiana jumanne Oktoba 16 kwenye uwanja wa Setsoto mjini Maseru, siku ambayo Tanzania 'Taifa Stars' akivaana na Cape Verde uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
IMG_20181013_194903_981.jpeg
IMG_20181013_203058_409.jpeg
 
Ifikie mahali Tanzania na sisi tuchukue achezaji wenye vipaji wasiokuwa na namba kwenye team zao za taifa kama vile Rwanda walivyofanyaga kwa Mafisango. maana hawa wachezaji wetu wa ndani ni wapuuzi kabisa sijawahi kuona.

Toa kocha wa kigeni weka mzawa mwenye uzalendo sio kocha mjuaji kama malaika.
 
Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes imejiimarisha kileleni kwenye kundi L katika michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019, baada ya kuichapa Lesotho mabao 3-0 kwenye uwanja wa Namboole mjini Kampala Uganda.

The Cranes wamefikisha alama saba baada ya mechi tatu, wakifuatiwa na Cape Verde yenye alama nne huku Tanzania na Lesotho wakiwa na alama mbili.

Ukurasa wa mabao ulifunguliwa na Emmanuel Okwi anayekipiga kunako timu ya Simba SC ya Tanzania katika dakika ya 11 kabla ya mchezaji Farouk Miya wa NHK ya Croatia kuandika bao dakika ya 36.

Ukurasa ulifungwa kama ulivyofunguliwa na yule yule Emmanuel Okwi kwa bao safi la kichwa katika dakika ya 63 ya mchezo.

Timu hizo zitarudiana jumanne Oktoba 16 kwenye uwanja wa Setsoto mjini Maseru, siku ambayo Tanzania 'Taifa Stars' akivaana na Cape Verde uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.View attachment 897036View attachment 897038
Hawa tayari wameshafuzu kimbembe kwetu sisi wanasiasa
 
Ifikie mahali Tanzania na sisi tuchukue achezaji wenye vipaji wasiokuwa na namba kwenye team zao za taifa kama vile Rwanda walivyofanyaga kwa Mafisango. maana hawa wachezaji wetu wa ndani ni wapuuzi kabisa sijawahi kuona.

Toa kocha wa kigeni weka mzawa mwenye uzalendo sio kocha mjuaji kama malaika.

Rwanda pia wamempa uraia Meddie Kagere.. Na sasa anarudisha fadhila kwao.
 
Okwi wa Simba ni yule yule wa Uganda Cranes, goli la kwanza kwa shuti kali mguu wa kushoto ni hatari kabisa

Naona Mkuu umerusha jiwe gizani.. Hahaha

Ila kwa hiki kiwango alichonacho ni faida sana kwa Simba SC. Katika mechi 2 za mwisho alizocheza kafunga goli 3.. Na namini 16/10 watakaporudiana ma Lesotho lazima ataongeza zingine.
 
Bado tunayo nafasi ya kufuzu, aliyetupiga kwao, tunampiga na sisi kwetu. Hizi kauli za kukatishana tamaa hazifai hata kidogo. Tuwatie moyo wachezaji wetu, maana ndiyo tuliokuwa nao kwa sasa. Na raha ya mbio in kumaliza wakuu. Viva Tanzania, Viva Taifa stars, mapambano bado yanaendelea, bado tunayo nafasi, tupambane tumkarishe Cape Verde taiga J.NNE. na watanzania wenzangu, hebu tujitokeze kwa wingi tuwape support wapambanaji wetu, hakika tunaweza. Mungu ibariki Timu yetu ipate ushindi hapo J.nne.
R.I.P TAIFA STARS
 
Ni hatari mkuu sembo ukiangalia namna alivyowachukua mabeki kabla ya kuachia shuti.

SimbaNguvuMoja..!
Naona Mkuu umerusha jiwe gizani.. Hahaha

Ila kwa hiki kiwango alichonacho ni faida sana kwa Simba SC. Katika mechi 2 za mwisho alizocheza kafunga goli 3.. Na namini 16/10 watakaporudiana ma Lesotho lazima ataongeza zingine.
 
Bado tunayo nafasi ya kufuzu, aliyetupiga kwao, tunampiga na sisi kwetu. Hizi kauli za kukatishana tamaa hazifai hata kidogo. Tuwatie moyo wachezaji wetu, maana ndiyo tuliokuwa nao kwa sasa. Na raha ya mbio in kumaliza wakuu. Viva Tanzania, Viva Taifa stars, mapambano bado yanaendelea, bado tunayo nafasi, tupambane tumkarishe Cape Verde taiga J.NNE. na watanzania wenzangu, hebu tujitokeze kwa wingi tuwape support wapambanaji wetu, hakika tunaweza. Mungu ibariki Timu yetu ipate ushindi hapo J.nne.
Mkubwa mimi sio mzalendo nyumbu nasema ukweli taifa stars haina kitu watakuja kufata point moja wale labda kikosi kibadilishwe.
LAKINI ulimwengu, himidi, kessy, mudathiri wakicheza wanaondoka na point hata moja wale jamaa
 
Exactly mkuu..! Wanajituma sana kwenye timu yao ya Taifa.

Huwezi kuwapanga wachezaji wa timu moja halafu utarajie ushindi...huwezi kumpanga Mwantika na Morris ambao ni wazito halafu utarajie ushindi...huwezi kumpanga mudahir na Himid pale katikati utarajie ushindi...wachezaji hawajitumi, wazito wanafuatana uwanjani mithili ya kumbikumbi...Hassan Kessy anakukuruka tu...hana nguvu...goli la pili kessy alizidiwa nguvu lakini Morris na Mwantika walikuwa hawapo kusaidia....Timu haina kiongozi uwanjani...Mwantika mipira ya kona kwa adui anapiga kichwa cha kuokoa baadala ya kudondosha mipira chini kwa kichwa...pengine mzuzu wake ulikuwa unamzuia kuona vizuri....niliangalia mechi yote ile..wachezaji hawako committed..Cape Verde walikosa magoli mengine mawili hivi...tungepigwa 5-0...
 
Moira in sayansi, pia Moira in mchezo was makosa. Ukifanya kosa mwenzio analitumia anapata goal. Kama uliicheck ile game taiga stars walifanya makosa kuanzia nyuma, viungo na forward pia. Ila hata jamaa walifanya makosa mengi pia ambayo kama tuna washabuliaji makini tungeweza kuscore walau hata goal moja. Point yangu ni kwamba hiyo game ya juzi imepita, Vila shaka mwalimu atafanya lililo ndani ya uwezo Wake upande wa ufundi kurekebisha alichokibaini. Tusikate tamaa, wala hakuna cha uzalendo nyumbu au Tembo, tukizamilia na kufanyia kazi mapungufu tulioonyesha last game, tukawa kitu kimoja, bado tunayo nafasi ya kutoboa. Tusiwakatishe tamaa wachezaji wetu na watanzania pia. Linapokuja suala LA timu ya taiga, hebu tuwe kitu kimoja, tuwe nyuma ya timu yetu, inshaalah Mungu anaweza awe upande wetu tukawatoboa jamaa. Chonde chonde rudisha moyo mkuu, kuwa mzalendo, hii ndiyo timu yetu ya taifa, kamwe Uganda crane haitakuwa timu yetu wala hao Cape Verde hawawezi kuwa timu yetu. Tuwape moyo wachezaji wetu. Tutatoboa tu.

Back
Top Bottom