Emmanuel Okwi awabwaga Mohammed Issa na Boniface Maganga katika tuzo ya mchezaji bora mwezi August 2017/18

Emmanuel Okwi awabwaga Mohammed Issa na Boniface Maganga katika tuzo ya mchezaji bora mwezi August 2017/18

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Mshambuliaji wa Simba ya Dar es Salaam, Emmanuel Okwi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Agosti wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Okwi alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam jana (Jumatano) na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa. Wachezaji wote hao timu zao zilishinda.

Walioshindana na Okwi katika hatua hiyo ya mwisho ni kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa pamoja na Boniface Maganga wa Mbao FC.

Pia Okwi amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga hattrick (mabao matatu katika mchezo mmoja) katika Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 16, ambapo hat trick hiyo alifunga ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kutokana na kutwaa tuzo hiyo, Okwi ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) atazawadiwa kitita cha Sh. 1,000,000 (milioni moja) na Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc.
 
Tuzo za kizandiki kupendeleana pendeleana aibu tupu.
Mchezaji kacheza mechi moja tu, watu wanawashwa kutoa zawadi aibu.

Tupambane kweli,tupambanishe kweli sio kupambanisha kwa hisia hisia tu.ni heri kutamka mwezi huu hakuna mshindi sababu mechi ni chache.

Kuliko kukurupukakurupuka na zawadi zenye maamuzi ya hovyo hovyo hovyo ni bora wangesema MFUNGAJI BORA wa mwezi.
 
37dc0ec70301356e81f18982ba693acc.jpg
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, limemchagua Emmanuel Okwi kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo yanaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali.

Taarifa hizo zimetolewa na Shirikisho hilo mchana wa leo na kusema wamefikia hatua hiyo baada ya Okwi kuwashinda wenzake wawili ambao ni Mohamed Issa wa klabu ya Mtibwa Sugar pamoja na Boniphace Maganga kutoka katika klabu ya Mbao FC katika uchambuzi uliofanywa jijini Dar es salaam jana Jumatano na kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.

My take: Okwi hakuwahi kutuangusha pale Msimbazi, kuanzia kuhusu fedha, na kandanda lake uwanjani. Hongera sana Okwi.
 
Emmanuel Okwi kaza umri unabisha hodi
 
Acha stori hata mechi moja tu inaweza tumika kupata man of the match
Tuzo za kizandiki kupendeleana pendeleana aibu tupu.
Mchezaji kacheza mechi moja tu, watu wanawashwa kutoa zawadi aibu.

Tupambane kweli,tupambanishe kweli sio kupambanisha kwa hisia hisia tu.ni heri kutamka mwezi huu hakuna mshindi sababu mechi ni chache.

Kuliko kukurupukakurupuka na zawadi zenye maamuzi ya hovyo hovyo hovyo ni bora wangesema MFUNGAJI BORA wa mwezi.
 
Acha stori hata mechi moja tu inaweza tumika kupata man of the match
Uko sahihi saana MAN OF THE MATCH kwa kiswahili ni "MCHEZAJI BORA WA MECHI"

Emmanuel Okwi ametangazwa kuwa ni MCHEZAJI BORA WA MWEZI KWENYE VPL.

mechi zilizochezwa ni 2 kwa mwezi AUGUST yy katumika mechi 1 ambayo alifunga goli 4.

Wenzake aliopambanishwa nao wamecheza mechi 2.

Hivi ni lazima kutoa MCHEZAJI bora wa mwezi hata wangesema mwezi huu hakuna MSHINDI.

Mchezaji bora wa Mwezi hupatikana kwa ubora ulio na muendelezo sio Leo kafanya vzr mechi inayofuata hakuna kitu.

Jiulize mechi moja INA muendelezo ktk kutafuta ubora!

Kwa hili kamati imekuwa na haraka mno.
 
Back
Top Bottom