Baada ya Okwi kuondoka Yanga niliwahi kupost hapa JF kuwa hatacheza Simba muda mrefu, ataelekea Azam kwa vile yeye anacheza na pesa tu; kala pesa Simba, kala pesa Yanga sasa ni zamu ya Azam kuliwa. Baada ya hapo ataelekea nchi nyingine ambayo mimi siijui, nijuacho ni kuwa hataendelea kuwepo Tanzania.
Ni maoni yangu kuwa nguvu ya Okwi ni pale anapokuwa Simba SC, nje ya Simba Okwi si lolote wala si chochote. Akienda Azam atakuwa amejimaliza mwenyewe, angalia Kipres wanavyo perform pale Azam, Kapombe naye si yule wa Simba na hata Kavumbagu siyo yule wa Yanga, hapo sijazungumzia Mwaikimba et al.
BR EA Okwi.