Endapo baadhi ya mataifa yangekuwa ni wanyama wa porini

Tsh

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2021
Posts
17,022
Reaction score
36,936
USA kitabia angefanana na Simba na comodo dragon. Ni hatari, jasiri, anavamia, anaumiza na anaogopwa kama simba, pia ana tabia ya kuvamia na kukung'ata akuachie sumu na kukufuatilia mpaka udondoke kama comodo dragon.


China kitabia namfananisha na Hyena. Fisi ni hatari, anavamia, ananyang'anya, mchokozi na pia muoga.


North Korea kitabia ni kama honeybedgar. Wanaogopwa hata na simba sababu ya mikwara.


Japan kitabia ni kama Fox. Fox hana madhara sana ila ana nafasi yake mwituni.


Urusi kitabia ni kama Mamba pia ana tabia za Tembo na vulture. Mkubwa kama Tembo na akiamini eneo ni lake yeye anapita tu kama Tembo alivyo na tabia ya kuvamia popote na kujimilikisha, pia ni hatari zaidi ndani ya mipaka yake, kama mamba alivyo hatari majini na anapotoka nje ya mipaka anakuwa na tabia ya kuvizia kama volture alivyo na tabia ya kuvizia kiumbe dhaifu.


German/England: Chui, anafanya mambo yake akimuhofia simba. Kama kafanya maamuzi na hakuna mti karibu wa kuyaficha maamuzi yake basi muda wote anaangalia simba asitokee kumvuruga.

 
Mkuu tanzania ingekua ni kicheche kwa tabia yetu ya mabeberu kujimegea na kuondoka
 
Tanzania tungekuwa ngiri aisee. Ngiri hana kumbukumbu, ukimpiga anakimbia halafu dakika chache anarudi hapo hapo. Zero brain
Haahahahaha. Mbona hatujipendi kabisa watanzania?
 
Tanzania tungekuwa Nyumbu, maana kila kitu tunafata mkumbo.
Nyumbu kila siku wanaliwa tu na wenye nguvu coz wanaminyama kibao lakini akili hawana.
 
Sisi ni kama Pono,mradi tunapata sehemu ya kulala bila bugudha msituni tunautandika usingizi kwa raha zetu.Hayo mengine tuwaachie kina Simba,Chui na Tembo wababe wacharuane.
 
Reactions: Tsh
Tanzania tungekuwa Nyumbu, maana kila kitu tunafata mkumbo.
Maana nyumbu kila siku wanaliwa tu na wenye nguvu maana wanaminyama kibao lakini akili hawana.
Yaani Hakuna Mtanzania anayeiona TZ kwa jicho tofauti? CCM ina kazi.
 
Sisi ni kama Pono,mradi tunapata sehemu ya kulala bila bugudha msituni tunautandika usingizi kwa raha zetu.Hayo mengine tuwaachie kina Simba,Chui na Tembo wababe wacharuane.
Hahaha ila Tuna nafasi yetu hata kama ni kidogo. Baba yetu Nyerere alifanikisha hilo kimataifa. Mm naiona TZ kama Sloth, tupo slow sana, rasilimali za ardhi nyingi ila hatuna nguvu ya kuzitumia hivyo wengine wanazitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…