Nauliza tu kwa wale wabobezi wa masuala ya Haki za Binadamu kama itakuwa ni halali kwa viongozi wa CHADEMA kuwazuia Wabunge wake wa Viti Maalumu ( Wanawake) kwenda kuapishwa na kushiriki vikao vya Bunge.
Iwapo CHADEMA itakuwa imepata 5% ya kura za jumla walizopigiwa wabunge wote basi wata-qualify kupata uwakilishi wa Viti Maalumu Bungeni na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi Mwenyekiti wa Bawacha Halima Mdee atakuwa miongoni mwa wabunge hao.
CDM itakuwa haijatenda haki pia watakuwa wamevunja Sheria za viti maalumu. Pia wanaume waache ubinafsi wakishinda wao ni sawa ikifika wanawake tu hawataki, so naona hapo Kuna gender discrimination flani