bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kama Katiba Inayopendekezwa Ingepitishwa, hakuna kipolo ambacho kingesalia kwenye kero za Muungano. Katiba hii ni nzuri sana kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Rais Kikwete ameyasema hayo leo wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mara ya mwisho akiwa Rais. Ameipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uongozi wa Jaji Joseph Sinde Warioba na Bunge Maalum la Katiba chini ya Mhe. Samwel Sitta. Amesema kinachosubiriwa ni Tume kuitisha Kura ya Maoni kwa ajili ya kuitimisha mchakato wa Katiba Mpya.