Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Ofisa lishe mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Dk Analace Kamala alisema minyoo husababisha madhara mbalimbali ikiwemo hilo la kupata matatizo ya akili.
Akiwasilisha mada katika semina kwa wanachama wa klabu ya waandishi Mkoa wa Dar es Salaam(DCPC) ya kuwajengea uwezo kuhusu kampeni ya mwezi wa afya na lishe ya mtoto, alisema minyoo inapojenga himaya ndani ya mwili wa binadamu huenda kuathiri mifumo mingine ikiwamo ya hewa, damu na ya fahamu, hapo ndipo mtu hujikuta akipata hadi matatizo ya akili.
Alitaja madhara mengine kuwa ni ukuaji hafifi kwa watoto, upungufu wa damu, kupungua uzito na kupata magonjwa yanayohusiana na ini pamoja na nyongo.
Ili kujikinga na minyoo, Dk Kamala, alisema ni vyema watu wakatumia vyoo na kuboresha usafi wa mazingira, kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, kukata kucha, kuchemsha nyama, samaki vizuri kabla ya kula nan a kutumia maji safi na salama wakati wa kula.
Mkurugenzi mtendaji wa TFNC, Eliphatio Towo alisema kampeni hiyo hufanyika Juni na Desemba kila mwaka.
Mwananchi