Endelea kuwatafuta mama lakini!!! Ni mwekezaji gani atakuja kuwekeza kwenye nchi iliyojaa uhalifu kila kukicha na umeme usio na uhakika?

Endelea kuwatafuta mama lakini!!! Ni mwekezaji gani atakuja kuwekeza kwenye nchi iliyojaa uhalifu kila kukicha na umeme usio na uhakika?

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Nimeshuhudia matukio ma4 ya uhalifu ndani ya wiki moja.
1. Ndugu yangu kabisa kavunjiwa duka wezi wamekuja na gari wamezoa kila kitu
(Tahadhari: kama una biashara ya vinywaji usilaze friji nje usiku likifanya kazi, wahalifu wanatumia umeme huo kukata milango na kofuli)

2. Ndugu ya jirani yangu kapigwa risasi na kuporwa pesa zote alizokuwa nazo,wakati anakusanya mauzo kwenye biashara zake. Jamaa kalazwa Muhimili hali mbaya

3. Sabasaba kwa Mpili barabarani kabisa wezi wamekuja wametoboa kwa juu ya duka na kuingia ndani,wamefanya yao wametoka na kusepa.

4. Mbagala Rangi 3 zimepigwa risasi kwenye duka la jumla wazee wamefanya yao na kuondoka.

Mama aliupiga mwingi sana mwanzo, anapambana kwelikweli kutoka nje ili kukaribisha na kuleta wawekezaji. Sa kwa uhalifu huu uliokithiri ni nani atathubutu kuja kuwekeza hapa?

Mwendazake hakuupiga mwingi na hakupata wawekezaji wengi lakini alidhibiti kabisa uhalifu,hatukusikia mambo haya yote. Kwanini mama asimbelee amri ile ile ya Magufuli?
 
Kwani wawekezaji kabla ya awamu ya 5 walitoka wapi iwapo awamu ya 5 ndiyo iliyodhibiti uhalifu? Au hapakuwa na wawekezaji kabla sababu ya uhalifu na wameanza kuja hao wachache wa awamu ya 5?
 
Bila ya Amani maendeleo ya kweli ni magumu sana
 
Back
Top Bottom