Eng.Hersi ataifikisha Yanga mbali na punde itaipiku Simba kwa ubora, save the date

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Jamaa sio mjinga, kwanza ni msomi, pili michezo ya kimafia anaijua, tatu anazunguka na timu ili kuwa karibu nayo, nne, sio mpigaji, tano, injinia anapenda sana sifa, sita, anaonekana kabisa ana uchungu na yanga.

Mimi kiukweli huyu Engineer japokuwa na ushabiki wangu lia lia kwa Simba ananivutia sana, jamaa ana mipango mingi na ya kiufundi, yeye haangalii ushabiki, kama ww una mapenz na Simba na unaweza kufanya kazi Yanga anakupa ajira lkn hakuingizi jikoni, mfano zungu pori, yuko yanga lkn mambo ya jikoni hashirikishwi ila anaambiwa tu atoe siri za kule alikotoka.

Eng.Hersi, kokote uliko,mimi mwana Simba kindaki ndaki nimefurahishwa sana na.mipango yako had ukaiondoa Club Africain ya Tunisia, kikosi hiki cha Yanga kwa hapa afrika cjui kama kuna wa kuwasumbua, endelee kuijenga yanga na kutufundisha sisi Simba maana tumekuwa kama mazuzu, we wachezaji wetu eti.Kibu, Nyoni, Bocco, Quattara, Akpan, Gadiel, Kanoute tunamsifia kumuita Putin wakat uchezaji wake aa kizamaaaani, cjui Mkude, Jimmson, Peter Banda.

Upuuzi mtupu

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Mmmh... Point yako ya msingi hasa ni ipi??! Yawezekana hata hao wakina Berkane hawatoshi kwa hao Yanga pia mana wamevuliwa ubingwa na wametolewa.. haha
 
Hao ndo mashabiki wa tz [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah
 
Kukosoa ni kazi rahisi sana ndo maana mashabiki wa matokeo wanajulikana kwa namna hiyo tu..!
 
Kila goti litapigwa hatimaye na wewe umeanza kushtuka taratibu na kuondoa tongo tongo machoni, Yanga tunaipa misimu 2 tu mbele kuwa timu tishio barani africa, yanga inajijenga kuanzia menejiment mpaka chini kwa wachezaji kiufupi uwekezaji wao sio wa magumashi ni uwekezaji wa ukweli umefata hatua zote muhimu na wanakwenda kuukamilisha kwa kishindo, sasa simba mpaka waje kushtuka na uwekezaji wao wa ujanja ujanja yanga atakuwa mbali sana yani tutegemee yale ya mamelodi na timu za Afrika kusini yakirudi Tanzania au yale ya Bayern munich na timu za ujerumani yakirudi Tanzania Save my post,
 

Mimi sikupingi na pia sikubaliani na ulichoandika kwasababu sijui undani. Ila wewe umeandika kana kwamba unaujua mambo ya ndani ya Yanga hivyo naomba unieleweshe.
1) kwa kipi kilichofanyika mpaka useme Eng. Hersi Said anajua michezo ya kimafia?
2) wewe ni shabiki wa Simba, je mipango ya kiufundi wa Eng. Hersi umeujuaje na una uhakika gani kama watendaji walioajiriwa hawaingii jikoni?
3) Yanga walipokuwa wanatangaza ajira, kigezo cha kupata kazi ilikuwa lazima uwe mwanachama wa Yanga, hivyo kama kuna mwana Simba amepata ajira kwenye klabu ya Yanga basi bila shaka kumekosekana uweledi kwenye kuajiri kwa vigezo na masharti vilishaanushwa.
4)Unaweza kunianishia ni mipango ipi unayoijua wewe Eng. Kaifanya ili kuitoa Club African?
5)Simba inamafanikio kimataifa kuliko Yanga kwa misimu takribani minne na mpaka sasa unaikosoa Simba ambayo imetinga hatua ya makundi na hujui uenda hata robo fainali au nusu ikacheza. Sasa je Simba wamefeli kwa lipi ukilinganisha na Yanga ambao tupo kwenye kombe la shirikisho?

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe.
1. Yanga imenyanyaswa sana na simba. Kwa hiyo itajitahidi kuondoa manyanyaso hayo mpaka yageukie kwa simba
2. Mwekezaji ni gsm na eng. ni mfanyakazi wa gsm. Anajituma kuonyesha uwezo wake. Kwa hiyo atafanya kila awezalo kuhakikisha anabaki kwenye nafasi yake.
 
Engineer wa wapi Herse Saidy???

UTOPOLO NI WATU WA AJABU SANA.

NABI WANAMWITA PROFESA!!!!!
SIJUI PROFESA WA NINI HATA HUWA SIELEWI.

shule Hana.
Wala HAJATUNUKIWA heshima POPOTE.

PROFESA Mihogo
 
Nakazia msimu huu tu yanga itafika mbali caf kuliko simba

Simba Kuna uswahili na hakuna uwazi Kama ilivyo kwa Yanga.

The way simba alifanya transformation ndio nilijua hapa hakuna kitu!
mpaka sasa Simba yupo mbali klabu bingwa wakati Yanga kashatoka, huwez wafananisha wakati wanacheza league tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…