Eng. Hersi Said usitumie lugha hii tena kwenye usajili

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Usajili wa wachezaji wageni: Kutumia social media kusema kuwa kila mchezaji mpya unaemsajili ni Bora kuliko aliyeko kwenye position Sasa sio lugha sahihi kutumiwa na kiongozi mkubwa ndani ya Yanga. Inawezekana hiyo ndiyo falsafa sahihi ya kusajili mchezaji mpya kwenye timu lakini sio lazima kiongozi aitamke hadharani na kwenye social media kwakuwa hii inavunja moyo wachezaji walioko kwenye nafasi hiyo Sasa.

Usajili ni kama kamali unayemleta anaweza asiwe Bora uwanjani kuliko uliyenae. Ni kweli kinadharia mchezaji mpya lazima awe Bora kuliko aliyeko lakini kiongozi mkubwa kama Rais wa club hapaswi kunena hayo kwa wachezaji wake waliomsaidia kuifikisha timu hapo ilipo. Kwanini mchezaji mpya kasajiliwa na wa zamani kaachwa au kaongezewa mtu mwingine inapaswa kuwa ni Siri ya jando ya bench la ufundi na uongozi, haizungumzwi hadharani. Wacha wadau wakapime wenyewe kazi zao uwanjani badala ya wewe kubeza walioko.

Naomba mfanye vitu kitaaluma, punguzeni mihemko mnapopata nafasi ya kuongea na wanahabari. Tafakarini athari kabla ya kusema chochote kwenda hewani
 
Usajili ni kama kamali unayemleta anaweza asiwe Bora uwanjani kuliko uliyenae. Ni kweli kinadharia mchezaji mpya lazima awe Bora kuliko aliyeko lakini kiongozi mkubwa kama Rais wa club hapaswi kunena hayo kwa wachezaji wake waliomsaidia kuifikisha timu hapo ilipo. Kwanini mchezaji mpya kasajiliwa na WA zamani kaachwa au kaongezewa mtu mwingine inapaswa kuwa ni Siri ya jando ya bench la ufundi na uongozi, haizungumzwi hadharani. Wacha wadau wakapime wenyewe kazi zao uwanjani badala ya wewe kubeza walioko.

Naomba mfanye vitu kitaaluma, punguzeni mihemko mnapopata nafasi ya kuongea na wanahabari. Tafakarini athari kabla ya kusema chochote kwenda hewani
Haji Manara ameshawaambukiza uropokaji. Hata Bumbuli kabla Haji bajaenda Yanga alikuwa ni mtu anayechagua maneno ya kuzungumza lakini naye siku hizi amekuwa mropokaji akiamini kuwa uropokaji ni kigezo cha kukubalika.
 
Bumbuli alikuwa so professional, siku hizi nae hajibu watu inavyopaswa kujibu, eti nae kaaza kujibu kwa kukera
 
Mumsamehe anatafuta kura za kutosha,unajua kwenye uchaguzi wabongo uwa wanapenda maneni yoyote yale mazuri kuyasikia hata kama sio ya kweli.
 
point moja nimeshika kuwa usajili ni kamari utajaza majina makubwa yanayoishia kuwa majeruhi na kuflop kushindwa kupafomu kama kule Kolo FC usajili uliopita ni majanga tupu hela yao ya usajili woooote imeliwa bure!!pesa ya waganga wa Kolo Fc imeliwa na Barabara nae kapiga zake!! uwekezaji wote = zero! Makombe yote kabatini Jangwani!!

Hersi tunamkubali sana ila kibinadamu inabidi awe makini na kauli za kuvunja moyo wachezaji, si vibaya akipitia video zote za Cedric Kaze zile anazoongea kabla ya mechi, jamaa anajua kutia moyo, mchezaji lazima apate morali
 
point moja nimeshika kuwa usajili ni kamari utajaza majina makubwa yanayoishia kuwa majeruhi na kuflop kushindwa kupafomu kama kule Kolo FC usajili uliopita ni majanga tupu hela yao ya usajili woooote imeliwa bure!!

Hersi tunamkubali sana ila kibinadamu inabidi awe makini na kauli za kuvunja moyo wachezaji, si vibaya akipitia video zote za Cedric Kaze zile anazoongea kabla ya mechi, jamaa anajua kutia moyo, mchezaji lazima apate morali
Unaposema simba haikuwa bora unalinganisha na mechi za matopeni a.k.a ligi kuu au kimataifa?.
Mimi nafikiri mpira ws bongo una hila nyingi.
Haiwezekani simba hiyo hiyo ipafomu vizuri kimataifa lkn nyumbani iwe mlenda...labda ni mambo yao ya kibongo, mambo ya dumba huenda wanashea mganga ndio anaamua msimu huu ni wa timu flani😂😂
 
mganga wa Simba wa Pemba kafeli nae wambadili kala pesa za bure, wachezaji wa Kolo FC wamekula pesa ya bure mishahara , Barabarani nae kala pesa za bure, mashabiki wamepoteza pesa za bure kuingia viwanjani!!
 
Hill lipo wazi duniani kote kila mchezaji ana level yake na tutasajili mchezaji mwenye uwezo zaidi ya waliopo kwasasa

Yanga sisi hatuna unafiki kama nyie makolo.... Huwezi kumsajili Akpan kutoka Pangani Tanga ukategemea akufikishe semi final kama ilivyo malengo yenu
 
Unaposema simba haikuwa bora unalinganisha na mechi za matopeni a.k.a ligi kuu au kimataifa?.
Mimi nafikiri mpira ws bongo una hila nyingi.
Haiwezekani simba hiyo hiyo ipafomu vizuri kimataifa lkn nyumbani iwe mlenda...labda ni mambo yao ya kibongo, mambo ya dumba huenda wanashea mganga ndio anaamua msimu huu ni wa timu flani[emoji23][emoji23]
Mie naona hata huko kimataifa haikuwa bora kihiivyo, sema timu zilikuwa zinaiogopa kwa sababu ya mafanikio ya miaka 3 ya nyuma tu. Zilikuwa zinacheza kwa kujilinda zaidi, zingecheza kwa kujiamini mbali na kuchukua kombe lao (robo) hata makundi asingetoboa.
 
Usajili wa wachezaji wageni: Kutumia social media kusema kuwa kila mchezaji mpya unaemsajili ni Bora kuliko aliyeko kwenye position Sasa sio lugha sahihi kutumiwa na kiongozi mkubwa ndani ya Yanga. Inawezekana hiyo ndiyo falsafa sahihi ya kusajili mchezaji mpya kwenye timu lakini sio lazima kiongozi aitamke hadharani na kwenye social media kwakuwa hii inavunja moyo wachezaji walioko kwenye nafasi hiyo Sasa.

Usajili ni kama kamali unayemleta anaweza asiwe Bora uwanjani kuliko uliyenae. Ni kweli kinadharia mchezaji mpya lazima awe Bora kuliko aliyeko lakini kiongozi mkubwa kama Rais wa club hapaswi kunena hayo kwa wachezaji wake waliomsaidia kuifikisha timu hapo ilipo. Kwanini mchezaji mpya kasajiliwa na wa zamani kaachwa au kaongezewa mtu mwingine inapaswa kuwa ni Siri ya jando ya bench la ufundi na uongozi, haizungumzwi hadharani. Wacha wadau wakapime wenyewe kazi zao uwanjani badala ya wewe kubeza walioko.

Naomba mfanye vitu kitaaluma, punguzeni mihemko mnapopata nafasi ya kuongea na wanahabari. Tafakarini athari kabla ya kusema chochote kwenda hewani
Aliyekuambia HS ana Akili ni nani Mkuu?
 
Mie naona hata huko kimataifa haikuwa bora kihiivyo, sema timu zilikuwa zinaiogopa kwa sababu ya mafanikio ya miaka 3 ya nyuma tu. Zilikuwa zinacheza kwa kujilinda zaidi, zingecheza kwa kujiamini mbali na kuchukua kombe lao (robo) hata makundi asingetoboa.
Lini Mtanzania ameanza kuongea ukweli na kubalansi mambo?
 
Mimi ni Yanga lialia ila Hersi yuko sahihi!anawaambia ili wajitume!wasibweteke!!limtu kama Mayele anajionaga kama CR7 hivi jinsi anavyojiona yuko juu!!

Bora hata alivyokosa Kiatu cha ufungaji bora maana angezidi kujiona keki ya Marble[emoji3]wakati hata Inonga tu anamtoa jasho la meno wakikutana je kimataifa na miamba kama al ahly atawaweza?!
 
Back
Top Bottom