OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wachambuzi wamechachamaa, wanapiga spana kila wakati. Hata wale wanaokupamba na kuopamba Yanga wamewageuka.
Machawa wako kimya, wamemwacha Afisa Habari analialia peke yake.
Sasa nakushauri fanya kama kawaida. Watie chochote kitu kabla mambo hayajawa mazito. Usipofanya hivyo kuna hatari huko mbele naiona. Nasema hivyo kwa sababu ajenda za kukupiga ni nyingi sana na hutoweza kuzijibu hasa ukizingatia ukweli kwamba umewekwa na huna uwezo.
Halafu wape hela vijana wa propaganda watengeneze propaganda mapema ili wailipue baada ya kipigo cha Tunisia.
Ni hayo tu kwa leo