Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Akitoa taarifa fupi ya Mradi huo Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng: Rogatus Mativila amesema Ujenzi wa barabara Wasso hadi Sale (km 49) ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mtandao wa barabara nchini kwa kujenga Barabara Kuu na za Mikoa kwa kiwango cha lami.
Eng: Mativila ameeleza kuwa Mkandarasi aliyejenga sehemu ya kwanza ya Wasso - Sale ni Kampuni ya China Wu Yi Co. Ltd ya China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 87.126, na kwamba mradi huo ulisimamiwa na TANROADS kupitia kitengo chake cha Uhandisi kiitwacho TANROADS Engineering Consulting Unit (TECU).
Aidha utekelezaji wa Mkataba wa kipande hicho cha barabara umegharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100, na mradi ulitoa jumla ya ajira 426 kwa wazawa na 21 wafanyakazi wa kigeni.