Engine oil kuzidi

shegacool2015

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
394
Reaction score
133
Habari za asubuhi wana jamvi...
Naomba kujuzwa madhara yakuzidi engine oil kwenye gari...namaanisha ikiwa ikezidi kile kipimo cha full...
 
kupungua na kuzidi yote mbaya ila kuzidi madhara ya kuzidi ni kwamba inauwezekano wa kupasua oil seal na hivyo kufanya engine yako kuvuja pale kwenye top cover
 
Habari za asubuhi wana jamvi...
Naomba kujuzwa madhara yakuzidi engine oil kwenye gari...namaanisha ikiwa ikezidi kile kipimo cha full...

oil pressure itakuwa kubwa hivyo itatafuta weak points za kutoa pressure hapo ndio oil seals zitaanza kupasuka na engine kuanza kuvuja oil sehemu mbali mbali.
au ikizidi sana itatengeneza air bubbles around crankshaft kwahi lubrication hapo itakuwa mbaya na kuua moving parts kama hio crankshaft yenyewe.
 
Thanks...asante sanaa kwa comments..hilo nimeli remark Leo bada ya kuona gari yangu ikitoa Moshi mweupe asubuhi..nilivo check oil nikakuta inazidi juu, nilivofanya service last week sikukagua mana Fundi namuamini...kwahiyo nifanye vp kupunguza? Or inabidi nimwage oil yote??
 
illegal migrant RRONDO #mchana jr
 
Last edited by a moderator:
illegal migrant RRONDO #mchana jr
 
Last edited by a moderator:

moshi mweupe ni dalili moja,hapo oil inapanda hadi kusipotakiwa....fungua SUMP PLUG na uipunguze OIL kiasi fulani then pima dip stick uone ipo level gani....sio lazima umwage yote ingawa kumwaga yote ingekuwa uhakika zaidi. una gari gani???
 
Toyota funcargo
 
Na inaweza kua ring piston nazo zimechoka au zimekakamaa maana haya magari used mara nyingi huwa na tabia ya ring piston na valve seal kukamaa kwa hiyo hurusu oil kuingia kwenye chamber ya piston.
 
Na inaweza kua ring piston nazo zimechoka au zimekakamaa maana haya magari used mara nyingi huwa na tabia ya ring piston na valve seal kukamaa kwa hiyo hurusu oil kuingia kwenye chamber ya piston.

yeah hilo linawezekana....
 
hio haizidi engine oil lita 4 tu....fundi akikuwekea aweke lita 3 pima kwanza kwenye dip stick then amalizie kuweka hio moja kama itakuwa haijajaa

OK thanks..ntajaribu kupunguza leo
 
Na inaweza kua ring piston nazo zimechoka au zimekakamaa maana haya magari used mara nyingi huwa na tabia ya ring piston na valve seal kukamaa kwa hiyo hurusu oil kuingia kwenye chamber ya piston.

Ntajuaj Kama ni ring piston,?
 
Toyota funcargo

Fungua sump plug gari ikiwa imetulia kwa muda baada ya kuwashwa au kuendeshwa punguza kama lita nzima (kwa uhakika) halafu rudishia plug yako, chomoa dip stick futa then pima oil level. Ongeza taratibu oil mpaka uoate ile max level kwa dip stick yako. Iwashe garikwa muda then iache itulie then check level again.

Moshi mweupe waweza endelea kuwepo mpaka iliyopita iungue yote ila ukizidi sana yaweza kuwa piston ring ingawa kwa gari kama hiyo sio tatizo rahisi kutokea
 
Pamoja na moshi mweupe gari itapoteza compression

Ni kama mtu aliyevaa viatu vilivyotoboka akatembea kwenye kokoto au mchanga wakati wa jua kali sana anakosa msukukumo wa kwenda haraka pamoja na kutumia nguvu mingi kujongea
 
Ni kama mtu aliyevaa viatu vilivyotoboka akatembea kwenye kokoto au mchanga wakati wa jua kali sana anakosa msukukumo wa kwenda haraka pamoja na kutumia nguvu mingi kujongea
Ha ha haaaaa acha vituko kaka
 
OLESAIDIMU asante sana mkuu na wadau wote mliochangia..nimelifanya zoezi na Moshi imeisha...asanteni sana
 
Last edited by a moderator:
Ndg acha ubahili peleka service kwa mafundi husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…