Engine ya pikipiki 150BM ni bei gani??

nyanda5

Member
Joined
Nov 25, 2014
Posts
49
Reaction score
40
Wadau habari~
Naomba msaada wa kujua bei ya engine ya pikipiki aina ya boxer maana chassis bado ni mpya kabisa lakini engine imekufa kutokana na matumizi mabaya ya kijana aliyekuwa anaitumia. Kuna rafiki yangu alinishauri kuwa ninunue engine ya FEKON nifunge kwani zinaingiliana sina hakika sana na hili naomba ushauri kwa mwenye uelewa please tusaidiane.
 
Nenda kwa wahindi pale kariakoo inategemea aina unayotaka.
 
Nenda kwa wahindi pale kariakoo inategemea aina unayotaka.

Mimi nipo Tabora mkuu, ninahitaji nipate ushauri nijue na gharama pia ili nione namna ya kufanya, kama gharama zitakuwa juu sana ni bora nikaachana nayo nikanunua pikipiki nyingine.
 
Mimi nipo Tabora mkuu, ninahitaji nipate ushauri nijue na gharama pia ili nione namna ya kufanya, kama gharama zitakuwa juu sana ni bora nikaachana nayo nikanunua pikipiki nyingine.
Injini bila fundi inafika laki tano mpaka sita,
 
Nenda alibaba.com search specification ya injini unayotaka...ukipata chunguza bei yake, unaweza kuwasiliana na muuzaji wa injini hiyo atakupa gharama za kufikisha injini hiyo Tanzania, hiyo gharama ya bei na usafiri jumla yake ongeza asilimia 87 ya kodi, ushuru na faida. Jumla kuu ndiyo itakuwa bei ya chini kabisa unayoweza kupata hapo Kariakoo...mara nyingi bei itakuwa zaidi ya hapo kama wauzaji wa kariakoo watakuwa hawajaingiza mzigo kimagendo. Sasa kokotoa gharama za kuifuata injini Kariokoo ukitokea Tabora....hiyo ndiyo itakuwa gaharama halisi ya injini uitakayo ya boxer.
 
Unaijua alibaba kweli...? Kule hawauzi kwa reja reja....
 

Nashukuru kwa maelezo ngoja nichek alibaba nione huko pia
 
Inawezekana kabisa kuweka ya fekon, haina garama napia spea zake ninafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…