Kwa uzoefu wangu wa kuangalia ajira na tenda kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari hapa bongo Civil engineering ina tenda na kazi nyingi sana ukizingatia nchi yetu inahitaji watu wenye utaalamu huo ktk projects mbalimbali za kujenga miundombinu mipya kama mabarabara, madaraja, vikwangua anga na hata projects mpya kama kujenga mji mpya wa kigamboni, airport na barabara za magari yaendayo kasi.
Kwa upande wa mshahara inategemea kampuni na kampuni lakini kampuni nyingi zinatoa kuanzia kilo 9 na kundelea, hii nazungumzia kutokana info nilizozipataa kutoka kwa wana ambao ni ma civil engineer, lakini pia usishangae kulipwa chini ya hapo maana experince nayo inamata na pia uwezo wako wa negotiate mshahara.