England 2- 1 Croatia

Somi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2009
Posts
3,921
Reaction score
4,858
Hatimaye waingereza wamelipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa wa Croatia. Wakitawala possession kuliko wa croatia kwa kiwango kikubwa wamewabwaga makamu bingwa wa Dunia kwa bao 2 kwa 1 Katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja maarufu duniani wa wembley . Wa Croatia walikuwa wa kwanza kufumania nyavu lakini kibao kiliwageukia mnamo dk ya 77 Jason lingard aliposawazisha na kapteni Harry Kane kuweka bao la ushindi nyavuni dk ya 85.
Kocha Gareth southgate Amezidi kufanikiwa huku akiwa na Kundi la vijana walio na vipaji, Hari na kujituma ambapo haijapata kutokea muda mrefu sana ktk historia ya Soka la uingereza.
Muda ndiyo utaelezea je kizazi Hiki ndiyo kitaleta kombe nyumbani au wataendelea kusubiri?
Ushauri : kocha southgate azidi kuwapa nafasi vijana hata wale waliochukua ubingwa wa Dunia kwa timu za vijana
 
Croatia inabidi waanze upya kizazi cha kina Modric muda wake umepita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…