ENGLAND: Unai Emery ateuliwa kuchukua mikoba ya Mzee Wenger

|Unai Emmery....
Ni swala la muda tu sasa bodi itamtangaza Unai Emery kama kocha mpya wa Arsenal..
1.Unai amcechukua vikombe 3 vya Europa League mfululizo..huku akiipiga Liverpool ya Jurgen Klopp kwenye fainali,2016.
2.Ni kocha ambaye anahitaji wachezaji wajitoe sana kwa timu..hana utani kwenye hilo-Tukumbuke haikuwa rahisi kuchukua vikombe akiwa na Sevilla timu ambayo ilikuwa na bajeti ndogo mno.
3.Yeye anasemwa kuwa ni kocha zaidi na sii meneja zaidi.Nadhani hiki ndicho kilichoivutia bodi ya Arsenal kumchukua yeye kwa sababu akiwa Sevilla alishafanya kazi kwenye nfumo kama wa Arsenal ambapo sasa-mkuu wa usajili wa wachezaji ni Sven Mislitant-while kule Sevilla alikuwa chini ya Monchi-na alifanikiwa!
4.Msimu wake wa kwanza PSG alishindwa kutwaa ubingwa-baada ya Monaco kuchukua.Baadhi ya wakosoaji wake wanadai huo ni udhaifu.Ila wanasahau kwamba timu ile ya Monaco iliitoa hata Man city ya Guardiola ktk hatua za mtoano UEFA champions League.
5.Anaongea kingereza kidogo tu-lakini alipokuwa Ufaransa ilimchukua muda mfupi sana kuongea kifaransa-hili linaonyesha kwamba ni mtu wa kujifunza lugha ngeni kwa haraka.
6.Ni rafiki mkubwa wa Pep...ni kati ya makocha wachache wanaoalikwa na Pep kwa glass ya mvinyo baada ya mechi...
 
Hata Zidane, anachaguliwa wachezaji na Florentino Perez.
 
Ueropa anaiweza sana nafikir arsenal wamemchukua kwa ajili hiyo
 
Yuko safi na ndo kocha wa arsenal
 
Coaches are hired to be fired
 
Atleast wameenda kwa mtu aliyejaribiwa tayari. Kumpa Arteta, Henry au Viera ingelikuwa kamari mbaya sana na ingeback fire tu. Sio kila mtu ni Zidane au Pep.
Angalau Giggs kidoogo alijaribu
 
Nacoweza kusema ni kwamba Arsenal wamelamba bingo kwa kumleta Unay Emery...ieleweke mimi ni Man Utd.
 
Nacoweza kusema ni kwamba Arsenal wamelamba bingo kwa kumleta Unay Emery...ieleweke mimi ni Man Utd.

Sio kocha mbaya ameshinda 3 Uefa cup, na Uefa Super Cup na timu ndogo sana (Sevilla) akishinda timu kubwa Kama Chelsea na Liverpool.

Inaonekana anauwezo mkubwa kuimprove wachezaji.

BTW chini yake Psg haikuwa timu mbaya.
 
Sio kocha mbaya ameshinda 3 Uefa cup, na Uefa Super Cup na timu ndogo sana (Sevilla) akishinda timu kubwa Kama Chelsea na Liverpool.

Inaonekana anauwezo mkubwa kuimprove wachezaji.

BTW chini yake Psg haikuwa timu mbaya.
Kwakweli ni mtu sahihi...PL itakuwa na changamoto za hapa na pale ambayo ni mambo ya kawaida hata Pep alikutana nayo.
 
chini yake Psg haikuwa timu mbaya.
Kwa mpunga ule, hata Moyes angefanya vyema pale PSG. Ngoja aone cha moto Arsenal - unapewa £50M na unaambiwa "fanya fanya maarifa hapo upate angalau 3 quality players'🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…