MJIMPYA
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 506
- 272
Ni ukweli kuwa sasa english imekuwa lugha ya dunia,
ni bahati mbaya tumejifariji na kiswahili na kushindwa kuwapa watoto wetu helimu nzuri hasa uwezo wa kuongea english kwa ujasiri kama kiswahili.
Nimefuatilia mtandaoni nikakuta China na maendeleo yao yote wanatenga fedha nyingi sana kuhakikisha watu wao wanajua english sawasawa, kuna vyuo vikuu vingi tu China vinatoa elimu kwa english na wamefungua milango kujichanganya na mataifa mengine ili kuhakikisha english inapewa kipaumbele.
Nchi kubwa kama Germany, Uholanzi n.k watu wao pamoja na kujua lugha zao wanajitaidi kujua na kuongea English, Italy nao hivyo hivo.
Uswiss nao wanazidi kujikita kwenye english pamoja na kuwa nchi tajiri na lugha zao za kitaifa.
Rwanda nao wameanza kiingereza juzijuzi ila wanahakikisha watu wanakiongea vizuri
Inasikitisha kuona nchi yetu ambapo English ni lugha ya taifa watu hawawezi kuongea kwa ujasiri hata wasomi wetu. Leo nimemwona Dr. Nchimbi mazishi ya Saitot akisoma hotuba ya english kwa hofu sana.
Yule mama wa Mbeya kwenye uchaguzi wa wabunge EA alipoona english aliingiwa na hofu akaamua kujito. Na wabunge wetu wengi ikitolewa agizo kuwa sasa tutumie english bungeni, wengi watakuwa mabubu.
Tuache kujifariji English haikwepeki sasa, nawashauri vijana hakikisheni unajua english ya kuongea kwa ujasiri, jipe mazoezi, kubali kukosea ili ujifunze.
Tunakoelekea soko linazidi kubana, ukiweza kuongea vizuri english kwa ujasiri ni mtaji wako mkubwa
Nawatakia heri na narudia tena English ni muhimu sana kwa sasa na wakati ulio mbele yetu, hakikisha unaweza kuongea english kwa ujasiri.
Nimeandika kwa kiswahili ili wengi waweze kusoma make wengine akiona makala ya kiingereza hata hasomi.