Enock, Henock, Enoko, Henoko - jina lenye hadhi na rahisi kukubalika

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Katika Biblia takatifu yapo majina mengi ya watu wa Mungu waliotenda Makubwa.
Jina la ENOCK, wengine huliandika HENOCK, Kwa Kiswahili cha Mvita ENOKO au HENOKO ni jina lililobeka sifa ya kipekee kwamba mhusika alikubalika na Mungu Hadi Muumba mbingu na nchi akaona isiwe taabu, huyu jamaa Kwa matendo yake hapaswi kufa kifo cha kibinadamu, akazikwa na kuoza Kwa sababu ameutumia mwili huo kumtukuza Yeye maisha yake yote. Biblia inasema, "HENOKO akaenda na Mungu maana alimtwaa" Mwa 5:24.

Leo Nataka nimwongelee HENOKO mmoja mchezaji, Beki anayeaminika na ambaye mamlaka inayosimamia soka nchini msimu uliopita ilimpa hadhi ya kuwa Mlinzi Bora miongoni mwa walinzi zaidi ya 200 wanaocheza ligi ya Tanzania.

Kwangu ni sahihi ni Bora miongoni mwa wengi. Lakini Leo niongelee kasoro/udhaifu alionao àmbao awali nilijua ni tukio la bahati mbaya.

Rafu aliyocheza dhidi ya mchezaji wa Yanga Salim Abubakar "Sure Boy" ilizua maneno mengi ambayo sina haja ya kuyarudia. Ni kweli ni faulu mbaya ambayo kama ingetimia ingeweza hata kusitisha uhai wa mwenzake maana mguu ungeweza kutua katukati ya utosi. Lakini pia kama mwamuzi angekuwa makini tukio hili lingeigharimu timu yake Kwa kucheza pungufu kwenye Mechi ngumu baada ya Kadi nyekundu.

Kama hiyo haitoshi, Mechi ya Jana ya kirafiki dhidi ya Al Hilal, HENOKO umerudia tena kitendo kama hicho japo wengi hawakukuona lakini ulifanya japo hakikuwa na madhara na ulijionya katikati ya kitendo. Tukio hili ulilifanya kwenye nusu yako karibu na katikati ya uwanja na nina imani unalikumbuka.

Sipo hapa kukuelekeza jinsi ya kucheza, lakini kukuonya kwamba matendo unayofanya kama masihara taratibu yatakupunguzia credit na mwisho utaonekana wa kawaida na thamani yako itashuka.

Wapo Wachezaji duniani waliotabiriwa Makubwa lakini aidha ukorofi au masihara yalipelekea mwisho mbaya wa maisha Yao ya soka. Paul Ince na Burton ni miongoni mwao japo wako wengi.

Punguza masihara ya kurusha mguu kihatarishi baada ya kuondoa hatari langoni mwako, kwani bahati haiwezi kuwa upande wako siku zote.

Wabilah tawfiq.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…