Enock Maregesi:- Utafiti na Majibu ya utafiti wa umri wa dunia

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kutokana na utafiti wangu wa siku mbili zilizopita, nimegundua kuwa si kweli kwamba dunia yetu ina umri wa miaka 6,000 ya mwanadamu. Bali, ina umri wa miaka 13,000 ya Mungu. Biblia yenyewe inasema kuwa siku 1 ya Mungu ni sawa na miaka 1,000 ya mwanadamu (Zaburi 90:4; 2 Petro 3:8).

Lakini sayansi ya dunia hii inasema kuwa dunia yetu ina umri wa miaka bilioni 4.5; ulimwengu wetu ukiwa na umri wa takriban miaka bilioni 14! Upande upi uko sahihi: sayansi au Biblia?

Kulijibu swali hilo vizuri, hebu tuanze na sayansi ya dunia hii; kisha tutapiga hesabu kwa pamoja, kuona ni upande upi uko sahihi au hauko sahihi:

Kwa kutumia sayansi ya upimaji wa umri wa vimondo, "radiometric age dating of meteorites", madini ya urari ("uranium") yana umri wa miaka bilioni 1 tangu yaundwe.

Madini ya zirconi ("zircon"), yanayotumika sehemu nyingi duniani kuwaletea watu bahati na utajiri hasa wanawake waliozaliwa Desemba, yana umri wa miaka bilioni 4.404 kutokana na kipimo cha kimondo.

Madini haya, zirconi, yanayojulikana pia huko Sirilanka kama "matara" kwa sababu yanachimbwa katika mji wa Matara, yanapatikana zaidi huko Australia (katika milima ya Jack) na Tanzania (katika mkoa wa Singida).

Lakini, madini ya kalisi yenye aluminiamu ndani yake ("calcium aluminium-rich inclusions") ndiyo yanayosemekana kuwa na umri mkubwa zaidi kuliko kitu kingine chochote kile duniani. Yana umri wa miaka bilioni 4.567. Kutokana na takwimu hiyo ya kalisi, wanasayansi wakahitimisha kuwa umri wa dunia yetu ni miaka bilioni 4.5! Lakini hawana uhakika wa asilimia 100.

Huo ni upande wa sayansi ya duniani kwetu. Sasa, kama nilivyoahidi awali, hebu tupige hesabu kidogo kwa pamoja ili tujue Biblia nayo inasemaje; ili tujue upande gani uko sahihi, hauko sahihi, au pande zote mbili kama ziko sahihi au haziko sahihi:

Siku 1 ya Mungu = Miaka 1,000 ya mwanadamu, ijapokuwa wengine wanaweza kuiunganisha 2 Petro 3:8 na uvumilivu.

Siku 365 za Mungu = Miaka 365,000 ya mwanadamu.

Hivyo, mwaka 1 wa Mungu = Miaka 365,000 ya mwanadamu. Sasa tuendelee kuanzia hapo:

Miaka 10 ya Mungu = Miaka 3,650,000 ya mwanadamu.

Miaka 100 ya Mungu = Miaka 36,500,000 ya mwanadamu.

Miaka 1,000 ya Mungu = Miaka 365,000,000 ya mwanadamu.

Miaka 6,000 ya Mungu = Miaka 2,190,000,000 ya mwanadamu.

Tangu Mungu amalize kazi yake ya uumbaji hadi leo ni miaka 6,000 ya Mungu, ambayo ni miaka 2,190,000,000 ya mwanadamu kama tulivyoona hapo juu.

Sasa, kumbuka kuwa, Mungu aliumba mbingu na nchi kwa muda wa siku 6; lakini siku ya 7 akapumzika. Kwa hiyo, kwa ujumla wake, Mungu aliumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa muda wa siku 7.

Hapo awali tumeona kuwa siku 1 ni sawa na miaka 1,000. Lakini pia, miaka 1,000 ni sawa na siku 1 (kulingana na 2 Petro 3:8, na kulingana na baada na wakati wa uumbaji).

Wakati wa uumbaji siku zote zilikuwa za Mungu; na vyote, siku 7 au miaka 7, kwa Mungu inaweza kuwa sawa na sekunde 1 tu. Lakini baada ya uumbaji siku zikawa za mwanadamu. Ndiyo maana baada ya mzunguko wa kwanza wa uumbaji kukamilika, Mungu anamwambia Enoch kuwa mzunguko wa pili wa siku 7 utakuwa katika mtindo wa miaka 7,000; ndiyo maana Enoch akazaliwa mwaka 3683 BC na kutwaliwa mnamo mwaka 3318 BC, akiwa na umri wa miaka 365.

Mwaka 3318 BC ni mwaka wa ishara ("symbolic"); ni siri ambayo Mungu alimpa Enoch wakati Enoch amemtembelea Mungu mbinguni, miaka 30 kabla ya kutwaliwa kwa Enoch. Katika kivuli cha AD, mwaka 3318 BC ni mwaka 3318 AD. Ukichukua mwaka 3683 BC (mwaka aliozaliwa Enoch) ukaujumlisha na mwaka 3318 AD (kivuli cha mwaka ambao Enock alitwaliwa) utapata miaka 7,000, ambayo ni namba muhimu sana inayohusiana na mwisho wa Dunia – yaani miaka 7,000 kamili tangu mzunguko wa pili wa uumbaji uanze rasmi mwaka 3683 BC. Hakuna anayejua kuwa dunia itaisha lini, lakini mwaka 3,000 AD utakuwa mwisho wa mzunguko wa pili wa uumbaji wa Mungu.

Kwa hiyo, wakati wa uumbaji, siku 7 zilikuwa sawa na miaka 7,000 ya Mungu. Sasa ukipiga hesabu kama tulivyopiga ile nyingine ya baada ya uumbaji hapo juu, miaka 7,000 ya Mungu ni sawa na miaka 2,255,000,000 ya mwanadamu.

Hapa duniani kwa sasa tupo katika mzunguko wa pili wa uumbaji wa Mungu. Tupo katika mwaka wa 6,000 wa Mungu tunaelekea katika mwaka wa 7,000 wa Mungu, kukamilisha mzunguko wa pili na wa mwisho wa uumbaji wake, utakaokamilika mnamo mwaka 3,000 AD.

Kwa hiyo, kupata umri halisi wa dunia yetu itabidi tuchukue miaka 7,000 ya uumbaji wa Mungu tujumlishe na miaka 6,000 ya baada ya uumbaji wa Mungu; ambayo ni 2,255,000,000 + 2,190,000,000. Ukijumlisha hapo utapata miaka 4,445,000,000, ambayo ni sawa na miaka bilioni 4.5 ya wanasayansi wa duniani kwetu.

Kwa hiyo Kibiblia, na kisayansi pia, Dunia ina umri wa miaka bilioni 4.5 ya mwanadamu! Yeyote anaweza kupingana na maelezo haya. Lakini huo ndiyo utafiti wangu kuhusiana na umri wa dunia yetu.

Kiteolojia, ukiulizwa kuwa dunia yetu ina umri wa miaka mingapi sema 6,000. Lakini kitaaluma, ukiulizwa sema bilioni 4.5.

-Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita
 
Bujibuji katika ubora wako sisi wasukuma na hayo makiswahili yenu wapi na wapi?
 
Umejitaidi kuchmbua lakini haya mambo mm Huwa nagenerate maswali mengi kidogo:;

Biblia na sayansi both are man made kwahiyo swala la kupata miaka sawa kote ni jambo la kawaida2

I don't think kwamba Kila kitu kilitokea the same time Dunia ilivo umbwa.. Mfano madini kutokea kwake lazima kuna some chemical, physical even biological presences zitokee Kwanza ndo madini flan yatokee, Hivyo bas Dunia ilikuepo even b4 those 4.5billions of years.

NB kamdanganye Bibi ako
 
Back
Top Bottom