EntomophagY, Je ni wakati wa kuwekeza kwenye wadudu?

EntomophagY, Je ni wakati wa kuwekeza kwenye wadudu?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Entomophagy ni neno la Kigiriki ambalo lina maana ya ulaji wa wadudu kwa binadamu na non human being.


Entomon ni Wadudu na phagein ina maanisha kula.

Zaidi ya makabila 3,000 duniani unaambiwa wana practice entomophagy.
Ulaji wa wadudu kwanza tuelewe haujaanza leo make ni back date huko Babu zetu walikuwa wanakula sana Wadudu, na Mabara kama
1. Amerika ya kusini na ya kati
2 Africa
3.Asia
4.Australia
5. New zealand
Wanatumia sana wadudu na kwa mjibu wa shirika la Chakula Dunuani asilimia 8% ya Population ya Dunia wanakula wadudu ambao kuna aina kati ya 1000 hadi 2000.

Baadhi ya Jamii hasa America na Ulaya ulaji wa wa dudu sio jadi yao na pia kuna wanao chukulia ni kama laana fulani ingawa now day Ulaya na hata Marekani wana Import sana wadudu wa kula.

Na EU tiyari isha ruhusu wadudu watumike kwenye vyakula vya mifugo kama Nguruwe na samaki na hata Kuku sasa.

Ila nchi kama Uholanzi, Denmark wao waliruhusu muda mrefu sana utumiaji wa wadudu hawa.

Asia ni mzalishaji mkubwa sana wa wadudu ambapo soko lake lipo Marekani na Ulaya pia.

BACK IN TANZANIA.

Kwa hapa Tanzania kuna baadhi ya makabila wanakula wadudu hasa.

1. Kumbikumbi ambapo makabila mengi hasa kanda ya ziwa wanakula sana na sio tu kanda ya ziwa hadi mwambao mwa ziwa Tanganyika kala Mkoa wa Kigoma kote huko wanakula sana kumbikumbi.

2 Senene pia wanaliwa sana.

3. Panzi pia wanaliwa sana.

Hao wote ni wadudu ingawa atill kuna species nyingi ambazo zinafaa kuliwa ila hatujaazila either kwa kuto kujua au kwa kujua then tukajisahau.

VYAKULA TUNAVYO KULA SAAA.

Ifahamike kabisa kwamba vyakula vyote kuanzia mtama, mahindi, viazi, Ulezi, uwele na vingine vyote vililetwa na wakolono hasa Wamisionary.

Sio asili ya Africa ingawa now day isha kuwa kama asili yetu.

KABLA YA HAPO.
Babu zetu walikuwa matunda mwitu now day hayapo make miti imekatwa imeisha.
Walikuwa wanyama mwitu kwa kuwinda na pia walikula Wadudu.

MITAZAMO YETU.

Wengi wetu kwa sababu zilezile athari za ukoloni tunaonelea kwamba kula vitu kama hivyo ni ushamba au kujidharirisha na tunasahau huo mchele uliletwa.

KWA NINI WADUDU NOW?
Kwanza wadudu kama Kumbikumbi au Senene au Cricket wana kiwango kikubwa sana cha Protein kikubwa mno.

Kumbikumbi ana hadi 60% hiki kiwango huwezi kukikuta kwenye chochote kile.

Wadudu wana virutubisho sana na niseme sio wote ni wa kula la hasha ila kwa wanao liwa wana virutubisho sana.

Kwa mujibu wa shirika la Chakula duniani yaani WFP tatizo kubwa la Tanzania sasa ni Utapiamlo.

Utapiamlo hausababishwi na ukosefu wa chakula bali unasababishwa kukosekana kwa baadhi ya virutubisho hasa Protein.

PROTEIN. Protein ndo chakula au Virutubisho ambavyo ni ghari sana iwe ni kwa binadamu au kwa mifugo.

LEO HII wa ngapi wana mudu kula samaki, au nyama? hivi ni vina protein kwa wingi na ni ghari sana.

SULUHISHO ni sisi kuwekeza nguvu pia kwenye wadudu hao ambao wana faida sana kwetu na sijui kama hao wanao kula kama walisha pata matatizo na kufa.

Kwa sasa pia kutokama na mabadiliko ya tabia nchi unaona mifugo inakufa sana, mazao yanantauka sana na Samaki kwenye maziwa ba mito zinapungua. leo hii ziwa victoria lina samaki wachache ajabu na pale pale Mwanza au Musoma kuna ambao hawawezi mudu kula samaki make ni ghari mno.

MAENEO KAMA YA WAFUGAJI NA ZILE KANDA KAME hapa ndo tatizo la utapiamlo liko juu sana tena mno.


WADUDU KWA MIFUGO
Mifugo yetu kama Kuku, samaki, nguruwe, Ng'ombe na kadhalika inapata changamoto kubwa sana ya lishe bora.

Leo hii protein ya kuwalisha ni ghari sana na ni ghari kwa sababu kuna ushindani kati ya binadamu na Mifugo

SOYA ya kuchanganyia kwenye chakula cha midugo iko juu sana kwa bei sabahu ni ushindani na binadamu na pia ukame.

Dagaa ndo kama hivyo no ni ghari kwa sababu pia wanasubiliwa na Binadamu.


Hivyo Wadudu wanaweza kuwa mkombozi wa chakula cha kulisha mifugo kama Nguruwe, kuku na Samaki na pia kwa wantama kama Mbwa.

NCHI kama South Africa walisha anza kujihami mapema sana na Wadudu na qana mashamba makubwa mno kwa ajili ya kuzalisha wadudu wa kulishia mifugo.

Nchi kama Uholanzi pia wanatumia sana kwa sasa wadudu kuchanganyia kwenye vyakula vya mifugo.

Mbali na Senene, kumbikumbi na Panzi pia wadudu kama Cricket na Blacksoldier wanaweza kuwa mkombozi mkubwa sana.

CRICKET hawa wanatumiwa kwa chakula cha binadamu na pi kwa mifugo huku BLACKSOLDIE wakitumika zaidi kwenye mifugo.


NB: Tuna aridhi ya kutosha tunao uwezo wa kuzalisha tani na tani za wadudu kwa ajili ya nifugo na binadamu na ku export pia.

BY CHASHA
images%20(9).jpeg
images%20(10).jpeg
images%20(9).jpeg
images%20(7).jpeg
Entovida-Large-Curry-Crickets%20(1).jpeg
po_bags_-_bw_32oz%20(1).jpeg
FB_IMG_1557673572333.jpeg
FB_IMG_1557673569400.jpeg
 
Back
Top Bottom