Tatizo siyo kuingilia anga mimi nilichokiona hii biashara ni sawa na biashara ya GNLD Tiashi na Forever living. Kwa taarifa yako wenzio huwa hawatozi kwenye mikutano yao kwa wale wapya wanaotaka kujiunga badala ya kulumbana na mimi ulipaswa kufafanua kama mkutano wako ni wa mafunzo au kutaka kuwaingiza watu kwenye ugavi? kama lengo ni kupata distributors kwa nini utoze pesa? hilo hujatueleza. Semina ya ujasiriamali Rombo ilikuwa free na kuna wana JF waliohudhuria na matangazo yangu yalikuwa yanaeleza kuwa semina ni free.