Kiteitei
JF-Expert Member
- Jan 14, 2009
- 1,595
- 1,540
aaaaaghrr!! niko na ka hangover ka jana, nimejipumzisha nikiwaza na kuwazua jinsi ya kureplace pesa niliyotumia jana bila mpangilio maalumu, mlangoni ngo ngo ngo, nauliza nani, naitwa jina......., ni mimi mama ....., natoka nje namkuta mke wa jirani yangu, uso umemvimba kichwani kavaaa kofia kuubwa,namuuliza kulikoni, nikahisi kapigwa nondo (niko mkoa ule almaarufu kwa nondo), naye akaniulza kwani jana hukuyasikia? nikajibu hapana... basii mdada wa watu kaanza kumwaga ya moyoni jinsi alivyopewa kichapo na mumewe wanayeishi naye miaka miwili sasa wakiwa na mtoto mmoja! mdada wa watu ameshaichukulia hali hii kama ni kawaida na ndio maisha yake ya kila siku!nimejaribu kumuhoji sababu eti kosa ni kuwa alikuwa anafua usiku! kama siku mbili hivi maji yalikuwa yamekatika!,namuuliza vipi hali hii umeshawahi kujadiliana au kulifikisha hata kwa wakubwa zenu! kajibu..yaani kwao wote wako hivyo, katikati ya maongezi anakuja mke mwenzie(mke wa shemeji yake) naye kavimba kama katiwa hamira..yeye anadai kapewa kibano juzi!!nawauliza washawahi kulifikisha mbele ya sheria, wote wanadai hapana na wanaogopa, wote wana mambo yanayofanana, jirani yangu alipewa mimba mwaka juzi akiwa form four na hakumaliza shule ikabidi aolewe, mzazi wake mmoja alishafariki na aliyebaki hana uwezo, mwenzie naye hakumaliza o level,wazazi wake wote wamefariki na hana ndugu mwenye uwezo,wote hawana kazi;hivyo waanajiona kama hawana msaada ila kilichobaki ni kuvumilia tu kipigo, nina incident nyingine inaendana na hii nikiwa dar last week.. why why sie wanaume tunawageuza ma punching bags hawa viumbe! kila mtu ana makosa but sidhani kama kipigo ndio suluhisho,niwashaurije hawa, ahh ngoja kwanza nitoke nikatafute supu washaniharibia siku hawa.