Enyi Watangazaji! Matumizi Yenu ya Haya Maneno Yana Walakin!

Enyi Watangazaji! Matumizi Yenu ya Haya Maneno Yana Walakin!

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Kila nitazamapo Tv au kusikiliza redio, nakumbana na matumizi ya maneno mawili ya kiswahili yanayoniacha hoi.Nawasikia wakitangaza: BoA ni benki itakayokuwezesha kuweza kupata mafanikio kwenye biashara zako.

Huo mtiririko wa maneno mawaili .......kuwezesha kuweza........ si sahihi hata kidogo kwa sababu dhana moja ya kuweza inarudiwa mara mbili!
Muundo huu utausikia sana kwenye vyombo vyetu vya habari ..... eg Shirika limewawezesha wakulima kuweza kupata mazao zaidi nk.
Rekebisheni Kiswahili chenu!
 
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"
 
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"

Baba V wewe noma!

Lakini hili balaa hata kwenye magazeti utalikuta. Makosa ya kisarufi hayana idadi

Wenzao China walipoona magazeti yanakosea kwa wastani mara 47 kwa kila gazeti ( wana herufi zaidi ya 40,000), waliona haja ya kuangalia mfumo wao wa elimu

Sisi tuna herufi 26 tu, makosa ya kimaandishi na kisarufi hayana idadi na wala wizara ya elimu haishtuki
 
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"[/UOTE] Baba V yaani hapo nilipobold ndo homa yangu ilipo. Mara eti Azam iliweza kufungwa bao moja na Yanga nk!
Yupo mtangazaji mmoja star tv ana huo ugonjwa wa kuweza. Akianza kutangaza nabadili chaneli.
 
Last edited by a moderator:
Hata humu jukwaani , tupo wengi sana tunaovurunda.Waungwana wakijaribu kuturekebisha tunakuja juu hili si jukwaa la lugha.
 
Tuna watangazaji, waandishi na hata viongozi serikalini ambazo wanaharibu mno lugha
Hivi kweli kabisa kwenye haya matangazo yao kwenye mabango, magazeti majarida, luninga nk nk wameshindwa kabisa kusema;
1: mabadiliko ni mimi ni wewe badala yake wanasema change ni mimi ni wewe!! Hili ni tangazo la twaweza yaani tunaweza
2:Tokomeza sifuri ndio Kiswahili fasaha lakini tunaambiwa tokomeza ziro/zero!! Tunauwa lugha yetu wenyewe
 
Mbaya sana. Mimi kinachonikera ni huyu mtangazaji wa jahazi anayewaita wenye ngozi nyeupe ni wakoloni. TCRA wanatakiwa kukemea hili haraka sana. Sidhani kama ni sahihi kwa sisi weusi kuendelea kuitwa watumwa. Vivyo hivyo sioni usahihi wa kuendelea kuwaita weupe wakoloni.
 
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"[/UOTE] Baba V yaani hapo nilipobold ndo homa yangu ilipo. Mara eti Azam iliweza kufungwa bao moja na Yanga nk!
Yupo mtangazaji mmoja star tv ana huo ugonjwa wa kuweza. Akianza kutangaza nabadili chaneli.

majeruhi mmoja aliweza kufariki wakati akikimbizwa hospitali.
 
Wafanyakazi wa strabag wanaojenga barabara ya morogoro road jana waliweza kugoma.
=====================
Ukipata Ujumbe wa chuki matusi futa delete kabisa
=====================
 
...
1: mabadiliko ni mimi ni wewe badala yake wanasema change ni mimi ni wewe!! Hili ni tangazo la twaweza yaani tunaweza...

Kwa hili nadhani ililazimu kubaki hivyo kwani tangazo lenyewe lina mwelekeo wa Kiswahili kinachotumika Kenya, ambako kama niko sahihi, ndiko chimbuko la kampeni hii.
 
Back
Top Bottom