Kila nitazamapo Tv au kusikiliza redio, nakumbana na matumizi ya maneno mawili ya kiswahili yanayoniacha hoi.Nawasikia wakitangaza: BoA ni benki itakayokuwezesha kuweza kupata mafanikio kwenye biashara zako.
Huo mtiririko wa maneno mawaili .......kuwezesha kuweza........ si sahihi hata kidogo kwa sababu dhana moja ya kuweza inarudiwa mara mbili!
Muundo huu utausikia sana kwenye vyombo vyetu vya habari ..... eg Shirika limewawezesha wakulima kuweza kupata mazao zaidi nk.
Rekebisheni Kiswahili chenu!
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"[/UOTE] Baba V yaani hapo nilipobold ndo homa yangu ilipo. Mara eti Azam iliweza kufungwa bao moja na Yanga nk!
Yupo mtangazaji mmoja star tv ana huo ugonjwa wa kuweza. Akianza kutangaza nabadili chaneli.
Kuna neno siku hizi limeshamiri "pahala".
Mkuu unaweza ukaichapa TV makofi kwa hasira, utasikia, "Alipigwa hadi AKAWEZA kufariki"[/UOTE] Baba V yaani hapo nilipobold ndo homa yangu ilipo. Mara eti Azam iliweza kufungwa bao moja na Yanga nk!
Yupo mtangazaji mmoja star tv ana huo ugonjwa wa kuweza. Akianza kutangaza nabadili chaneli.
majeruhi mmoja aliweza kufariki wakati akikimbizwa hospitali.
...
1: mabadiliko ni mimi ni wewe badala yake wanasema change ni mimi ni wewe!! Hili ni tangazo la twaweza yaani tunaweza...