Pre GE2025 Enzi ya awamu ya kwanza watu tishio walikuwa wanawekwa kizuizini, siku hizi mambo ni tofauti!

Pre GE2025 Enzi ya awamu ya kwanza watu tishio walikuwa wanawekwa kizuizini, siku hizi mambo ni tofauti!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Nakumbuka Mzee Tuntemeke Sanga aliporudi nchini kutoka ughaibuni akaulizwa na Mwalimu unataka cheo gani? Akasema Urais. Akapelekwa kizuizini kwao.

Mzee Christopher Kasanga Tumbo alipopishana na watawala akaishia kupelekwa kizuizini.

Bibi Titi Mohamed alipokula njama mwaka 1969 ya kutaka kumpindua mzee mchonga akaishia kizuizini mpaka mwaka 1990 akachiwa huru.

Huu utaratibu ulikuwa mzuri maana ulijali utu wa mtu. Hali ya sasa inatia mashaka, mtu unapokonywa utu wako!

Muwe na Jumapili njema!

Pia soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Natamani siku zirudi nyuma tutawaliwe na wajerumani Tena.Kwa Sasa nchi umeharibika sana.mauaji yanayofanywa na hii serikali haijawahi kutokea hapo kabla .Mtu anatekwa mchana kweupe na gari za serikali V8 land cruiser likiwa na namba za serikali
 
Back
Top Bottom