N-handsome
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,453
- 560
Akyanani hili neno...................KIPOLI......limenikumbusha mbali saaanaaaaa.........JAMANI SHULE KULIKUWA NA RAHAAAA SAAANAAAAA
Wewe chijana umenikumbusha mbaaliii!!!
Nimekumbuka sana maisha ya sekondari fulani ambapo tulikuwa na majina kibao kwa walimu wetu. Nakumbuka mwalimu mmoja tulimwita Kifaru na mke wake tukamwita Kidedea kwa jinsi miili yao ilivyokuwa mikubwa. Chakushangaza majina hayo walikuwa wanayafahamu. Watundu wachache wakambadilishia jina huyo mwalimu wa kiume nalo akalifahamu. Basi siku moja akajilipua morning assembly. Akasema, vijana kumezuka mtindo wa kupeana majina hapa shule. Mliniita Kifaru, nikakubali. Mke wangu mkamuita kidedea, nikakubali; sasa hili jina la popobawa litakwenda na mtu!!!
Basi alikuwa akipita karibu na mabweni ya wanafunzi watu wanaanza kuita kwa sauti POPOBAWA popobawa na asifanye kitu.
Baadaye alikuja mwalimu mkuu mmoja mkorofi sana, hakiyanani alinifanya nitoroke parade za asubuhi kwa jinsi alivyokuwa akiadhibu. Siku mmoja alimkoa jamaa wa nyuma yangu konzi zito ambalo lilihamishia maumivu kwangu na siku hiyo nikasoma kwa shida kwa ajili ya ule mlio. Huyo mzee nasikia alishafariki, kama kweli r.i.p Msasa. Huyo tulimwita Hitler na makamu wake alipewa jina la Natenyahu ambapo yeye wenyewe alikiri kapewa jina zuri.
Kuna jamaa lingine sijui mzima ama sio mzima, yeye alijiita UNYAMAUNYAMA maana ukiwa na soo nae mnamalizana kwa fimbo ama ngumi. Na hata ukimshinda hana kesi na wewe bali anajipanga upya. Hili jamaa lilikuwa linakuja kutuamsha saa 11 alfajiri kwamba tutoke kwenye magorofa ya serikali na kwenda kufanya usafi. Lilipenda kusema mkitaka raha jengeni zenu!!! Wanafunzi nao wanamtukana kuwa wenzake wamelala na wake zao yeye anakimbizana na wanafunzi kwa kuwa mke wake kipoli. Na yeye anajibu hata km kipoli mimi najali mchezo. It was real funny with those guys.
Kulikuwa na huyu pia
'Kocha'..... huyu hachapi fimbo lakini adhabu zake lazima utoe chozi (push ups, kichurachura nk).
Nawakumbuka sana wafuatao enzi zilee za mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa tisini
1. Kinyakanyaka............ akianza kukuchapa fimbo anataja .....BLOOD KINYAKANYAKA
2. Mbungi wa umeme............ AKIKUKAMATA ALIKUWA ANASEMA...UNANILETEA MBINGI MIMI
3. Brigedia mwakalindile...........WIKI YA ZAMU YAKE ILIKUWA NI BALAA
4. Olu wa kiingereza
5. People ..........KILA BAADA YA NENO MOJA AU MAWILI LAZIMA ASEME ..... PEOPLE
Mi nilikuwa form 1B (kwa mchili) and then group four niliishi D2 seuta mwanzo hadi namaliza............Pia kulikuwa na "Per T T" yule mwalimu wa Physics ( Engineering Science) form I kila saa alikuwa anapenda kusema "per time what...?? part time taken, par t".
Huyu jamaa alikuwa anapenda totoz sana alikuwa anaramba wasichana wazuri wote wa form I.Wakishapanda madarasa hana habari nao anasubiri form I tena.
Duh kumbe IFUTESCO( Ifunda Tec Sec School) tupo wengi...
Nilikuwa bweni la Chabruma pale F5 na F6
BTW: Per T T ni marehemu sasa, Ukimwi umeua /unaua sana walimu wetu aisee!,
Its so sad. Amefariki lini? Nakumbuka niliwahi kukutana nae hapo baraza la mitihani (nadhani mwaka 2004 hivi).
Ni kweli walimu wengi wameshawahi mbele ya haki kwa hili gonjwa wangali bado vijana.
Lol!...kwa ma-veterans wa Ifunda salute kwenu!
Ile shule ilkuwa ni KAMBI ndogo ya JESHI?, form two's walikuwa na uwezo wa kufunga bweni moja na kuwatembezea kichapo wote, forget about form one ambao walikuwa ni zaidi ya watumwa!
BTW: Per T T ni marehemu sasa, Ukimwi umeua /unaua sana walimu wetu aisee!, huyu alikuwa ukiwa na soo naye sepa halafu bdae ukiridu msifie kwa hasira zake, 'kuwa mwl ungeniua pale thats y nikakimbia, ww ni noma mwl, lazma alegee, au mmtume demu akajieleze lazma atawapotezea..lol!'...
Wewe chijana umenikumbusha mbaaliii!!!
Nimekumbuka sana maisha ya sekondari fulani ambapo tulikuwa na majina kibao kwa walimu wetu. Nakumbuka mwalimu mmoja tulimwita Kifaru na mke wake tukamwita Kidedea kwa jinsi miili yao ilivyokuwa mikubwa. Chakushangaza majina hayo walikuwa wanayafahamu. Watundu wachache wakambadilishia jina huyo mwalimu wa kiume nalo akalifahamu. Basi siku moja akajilipua morning assembly. Akasema, vijana kumezuka mtindo wa kupeana majina hapa shule. Mliniita Kifaru, nikakubali. Mke wangu mkamuita kidedea, nikakubali; sasa hili jina la popobawa litakwenda na mtu!!!
Basi alikuwa akipita karibu na mabweni ya wanafunzi watu wanaanza kuita kwa sauti POPOBAWA popobawa na asifanye kitu.
Baadaye alikuja mwalimu mkuu mmoja mkorofi sana, hakiyanani alinifanya nitoroke parade za asubuhi kwa jinsi alivyokuwa akiadhibu. Siku mmoja alimkoa jamaa wa nyuma yangu konzi zito ambalo lilihamishia maumivu kwangu na siku hiyo nikasoma kwa shida kwa ajili ya ule mlio. Huyo mzee nasikia alishafariki, kama kweli r.i.p Msasa. Huyo tulimwita Hitler na makamu wake alipewa jina la Natenyahu ambapo yeye wenyewe alikiri kapewa jina zuri.
Kuna jamaa lingine sijui mzima ama sio mzima, yeye alijiita UNYAMAUNYAMA maana ukiwa na soo nae mnamalizana kwa fimbo ama ngumi. Na hata ukimshinda hana kesi na wewe bali anajipanga upya. Hili jamaa lilikuwa linakuja kutuamsha saa 11 alfajiri kwamba tutoke kwenye magorofa ya serikali na kwenda kufanya usafi. Lilipenda kusema mkitaka raha jengeni zenu!!! Wanafunzi nao wanamtukana kuwa wenzake wamelala na wake zao yeye anakimbizana na wanafunzi kwa kuwa mke wake kipoli. Na yeye anajibu hata km kipoli mimi najali mchezo. It was real funny with those guys.
mnanikumbusha neno " SHIKWAMBI" hili lilikuwa neno la kubuni tu pale Moshi Tech.
SHI - Shiba
KWA - Kwa
MBI - Mbinu.
Pia maneno kama TOP LAYER - Utando wa juu wa maharage yaliyoungwa kwa wese.
ZERO - kwenye mabweni ya wasichana
Kuna mwalimu wa Vijana - alikuwa hatari kwa super six akikukuta hujakimbia mchakamchaka soo lake afadhali ukamatwe umebaka - ni super six kila siku wiki nzima na adhabu kali ya kufukua visiki kule orchard (shamba la michungwa)