Enzi zile za kuangali movie kwenye mabanda ya video (1990s)

Enzi zile za kuangali movie kwenye mabanda ya video (1990s)

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
1,926
Reaction score
2,797
Miaka ya tisini (1990s) swala la kumiliki television a.k.a video ilikuwa ni tatizo ni familia chache sana ambazo zilizokuwa na uwezo wa kumiliki, hivyo kuifanya ni bidhaa hadimu kwenye mitaa ya uswahilini.Nakumbuka miaka hiyo tukiwa tumepangisha maeneo ya Kinondoni mtaa wa togo karibu na kipindi hicho baa alimaarufu kinondoni bar karibu na baa nyingine ikiitwa vijana bar.Mtaa nzima ni familia chache sana zilizokuwa na television, sana sana ni kwa zile familia zilizokuwa na asili ya kiarabu ndio zilizokuwa nazo,sisi wengine ilikuwa ni majanga.Kutoaka na hali ya familia kutokuwa na uwezo wa kununua mayanki wa kipindi hicho ilitulazimu kwenda kutazama movie kwenye mabanda ya video.

Nakumbuka kwa kuwa nilikuwa mpenzi wa video nilikuwa naenda kutazama movies kwenye hayo mabanda na kutokana na udogo wangu nilikuwa sina pesa ya kiingilio ambacho kilikuwa kati ya shilingi 20 mpaka shilling 30 kwa picha moja, tabia ya udokozi nyumbani ikaanza rasmi.Ilikuwa kwenye matumizi ya nyumbani lazima nipite na shilingi 200 au 100, nilikuwa nachezea bakora mno lakini dhubutu utamu wa movies sikuwaelewa kabisa.

Kumbukumbu zangu zinaniambia ratiba ya siku ilikuwa inaanza saa 3 asubuhi ambapo walikuwa wanaanza kwa kuonyesha nyimbo mbali mbali kama za wakina yondo sister,defao,koffie olomide,bozi boziana,pepe kale na wengine wengi.Baada ya hapo ratiba inawekwa kwenye ubao wa movies ambapo lazima movie ya kihindi ianze huku ikifuatiwa wa zile za kizungu kutokana na upenzi wa kuangalia hizo movie niljikuta nakuwa ndiye mtoa simulizi nikifika shuleni na kuongopeana na wasio jua wenzangu.Vilevile niliweza kuyajua majina mengi ya wacheza sinema kutokana na kutokujua title nyingi za movie kutokana na lugha gongana.

Ratiba ya haya mabanda umiza ilikuwa inaishia mara nyingi saa mbili ya usiku baada ya hapo ule muda muafa wa watu wazima pekee kuangalia ndio ulikuwa unaawadia. Muda wa kuweka picha za wakubwa hali maarufu pilau au picha za X.Hapo madogo wote tulikuwa tunatimuliwa wanabaki watu wazima tu.Njia pekee ya kuangalia ilikuwa ni kwa kupiga chabo ila usiombe ukamatwe utaishia kuchezea mbata za kutosha..mitama kama yote na makonzi sana.Nakumbuaka kuna siku moja nikiwa nimekaa back benj natazama pilau mara pup anaingia baba yangu mdogo…dah nillikosa amani muda wote wa kutazama pilau..hata baada ya kutoka nilikuwa nawaza kama hajaniona,lakini nilisave siku hiyo nahisi hakuniona au pengine nayeye baada kuniona aliona nishai kuniwashia kwa kuwa nayeye alikuwa anaangalia.

Kutokana na usumbufu huo nilijiapiza nikija kuwa mkubwa na nikiwa nafedha nitanunua video yangu nitakuwa naangalia muda wote.Japo lengo limetimia lakini hata muda wa kuangalia sina kutokana na ubize wa majukumu ya kila siku nashia kulipia vingamuzi tu.

NB; HEBU TUPIANE EXPERIENCE VIJANA WENZANGU WA MIAKA HIYO
 
Kweli mkuu hata mm nilipokuwa mdogo nilisema siku nikinunua tv muda wote ni kuangalia lakin baada ya kununua sina hamu hata huo muda sinaga zaid nimekuja kuwa mpnz wa kusikiliza music zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu hata mm nilipokuwa mdogo nilisema siku nikinunua tv muda wote ni kuangalia lakin baada ya kununua sina hamu hata huo muda sinaga zaid nimekuja kuwa mpnz wa kusikiliza music zaid

Sent using Jamii Forums mobile app

kama mimi enzi za video games ndio zimeingia ,tulikua tunaenda kucheza game kwa watu pc zilikua chache, na ukienda unaezapewa dakk 10 tu za kucheza then unaangalia mwenzio akicheza for 6 hours
nilipopata pc sasa games nilizichoka


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua na tuliyeitana mchumba wangu mwenyewe tukienda kwenye mabanda ya video tunakaa kwenye kagizagiza ananifunua sketi aangalie mapaja na kunishika nyonyo .. utoto bana

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom