shukurani ya serikali za kiafrika ni mateke. Kwanza utumikie taifa miaka 40 ya maisha yako, ukinunua gari wananchi wanapiga kelele hata hawajali umetumikia nchi kwa muda gani, ukipita barabarani unazomewa kuwa wewe unaiba bila hata ushahidi wa kutosha, ukistaafu unaambiwa uripoti mahakamani kuwa umeitia hasara serikali yako halafu wananchi wanashangilia bila hata ushahidi ama uamuzi wa mahakama.
Je kwa mtindo huu, nani atatumikia taifa kwa moyo wote? Pili waheshimiwa na mafisadi wa epa waliorudisha pesa waliyoibia serikali majina yao hayatajwi. kumbe mwizi akiiba akarusha alichoiba si mwizi tena. Watanzania tuamkeni usingizini. Kikwete anafanya kiini macho. Mramba, yona na mgonja wameitia serikali hasara na wamefikishwa mahakamani. Zhakia meghji aliye saini check ya bilioni 31 akampa ulaji balali yuko huru na hakuna mashtaka juu yake. Jee? Kati ya zakhia na (mramba, yona na mgonja) nani katia hasara kubwa serikali? au bilioni 31 ni ndogo kuliko bilioni 11?
mwizi ni yule aliyekamatwa ... Kila kitu kina wakati it took 3 years to investigate mramba & co. Huwezi jua pengine hata lowasa & co wako under investigation na muda ukifika watapanda kizimbani
lowasa na richmond boys, wako huru na hakuna mashitaka juu yao. Wametia serikali hasara ya bilioni 170. Wako huru na kukamilisha kiini macho, waliopoteza bilioni 11 wako mahakamani. Ccm haiko mahakamani pia lakini watanzania wanashangilia ati mafisadi wako ndani. Mtaamka kesho kujua kuwa hiki ni kiini macho.
huwezi jua pengine hata lowasa & co wako under investigation na muda ukifika watapanda kizimbani
kikwete anawajua marafiki zake waliorudisha billioni 70 za epa na majina yao hataki yatajwe kwa sababu ni jamaa zake na anakula nao. na yeye akimaliza muda wake tumfikishe mahakamani. majaji wetu nao wanatutia aibu. Kesi ya watu watatu ya bilioni 11 dhamana yake ni ya watu watatu. Cha ajabu mtu mmoja anatakiwa atoe nusu ya hiyo pesa kana kwamba nashtakiwa pekee kwenye kesi tofauti. Au ndiyo kukomoana?
Jitu patel ni ndugu kabisa na shubashi patel, subashi patel kwao lugoba, jamaa wa karibu kabisa na muungwana wetu.... Na ametinga kisutu.
watanzania tuamkeni. Kikwete ni mmoja wa epa pia. Mafisadi wako wapiiiiiiiiiiiiiiiiii.?
watu wengine bwana, ulitaka hadi mbowe awe rais ndio ujuwe kazi inafanyika ...