EPA na mambo yake

Rostam hajafungwa na hawezi fungwa unless it becomes absolutetely necessary...as in it becomes certified (with some hard evidence) kwamba jamaa kapiga tukio.. nikama kusema Apson afungwe.. that can never and will never happen...EVER

Mkuu naomba tusihalalishe wizi. Tusimamie sheria, hizi habari za kusema hakamatwi mtu tunzaijua, sasa hata kama ni firauni asikamatwe ka sababu hakamatiki? Hard evidence???? Ipi hiyo tena ya chuma au??
 

Huyo Davis Kamungu (DAvies Mosha) Aliwahi kutoka kwenye michuzi huku michuzi akisifia Bongo Tambarare kama utakumbuka hiyo statement ilizua mjadala mkali sana kuhusu hali halisi ya bongo
Nikikukumbusha alikuwa amepiga picha na lile AUDI Q7 yeye anaongea na simu
Ni zamani kudogo.
 

Kumbe ndiye mweye kampuni hii: Home
 



Kuku mjanza hukamatwa kwa tundu bovu/mtego mbovu. Amepata utajiri kwa kiujanja ujanJa na utaisha kiujanjaujanja. Tena siku za usoni nilipita maeneo ya Mto wa Mbu ana hotel (Njake Hotels and Tours) pale na kituo cha mafuta. Hotel kwisha, tena inaonekana imefungwa au ndo wateja hakuna. Maana nasikia alikuwa anategemea wazungu, sasa tena unajua wazungu wako sensitive hali hiyo ime shift demand!!!!

Ila tu utajiri aliokuwa nao tayari ungemtosha, tatizo ni tamaa!!!!!

At the same time yeye anasema alidanganywa kuwa ni clean business!!!! Sasa swali linakuja hivi "Kama ilikuwa pesa halali ungeambiwa utoe pesa nyingi uwalipe waliokusaidia kuzipata, Balali na vijana wake? Na pia ni lazima kujiuliza, je hili siyo deni ni fedha ya bure!!!??? Kuna kitu kama fedha ya bure ambayo hutakiwi kurejesha kama vile mkopo utakiwavyo? Sasa hapo sielewi mshauri wake kibiashara ni nani au ni wale wazee ambao kila kitu wanajiammlia hata mke hausishwi? " Majibu ya haya yote anayo Njake na mkewe na watoto. Watoto amesomesha Uingereza, sasa sielewi anawapa nafasi gani ya kutoa mawazo katika biashara au tena FISADI NAYE ANAZAA FISADI? KAZI KWAO.
 

Huyu Davis Kamungu hana hela yoyote wala huyo Godfrey Mosha.Tusichanganye hapa hawa watu na Davies Mosha ambaye ni tajiri wa mafuta n.k. Tunashindwa kuweka mengi hapa kuhusu uhusiano wa hawa watu na changanyikeni complex kwasababu suala hili liko kwenye mikono ya sheria.

Godfrey Mosha na Davis kamungu walitakiwa ama kudeposit kiasi cha shilingi milioni 240 au kukabidhi hati ya nyumba yenye thamani hiyo.Thamani ya nyumba iwe imethaminiwa na mthamini wa serikali sharti ambalo walitimiza kwasababu tayari walikuwa wana hati hizo majumbani kwao.

Tofauti ni kwamba watuhumiwa wengine walianza kuhaha kutafuta wathamini majengo wa serikali mara baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mahakama na hiyo ndiyo imepelekea washitakiwa wengi wa epa kushindwa kupata bail mapema.
 
Jamani mvute subira vitu vizuri havitaki haraka. Ni wazi kuwa Rais na serikali yake imedhamiria kufanya kweli kwa EPA mkumbuke uchaguzi mkuu hauko mbali sasa CCM imepata pa kutokea na ninawahakikishia vigogo wa juu watakuwemo tu sema kamatakamata hii inakwenda kwa mahesabu ili tu wasijeshtuka na kukimbia nchi (kama bado hawajakimbia) ila wote waliohusika watawekwa ndani mmoja baada ya mwingine.


Heko Kikwete hapa umecheza ni wazi kuwa kukosa ubunge Tarime kumekudhihirishia ni kiasi gani watu wamechoshwa na miyeyusho ya serikali yako so kwa EPA jisafishe mwanangu usijeula wa chuya..............2010
 
wakuu,kuna nyuzi IPPMEDIA yenye tittle ''Soo la EPA:Gavana Ndullu atajwa!"
sikuweza kuisoma,wenye access ya mtandao watugawie tafadhari.
 
wakuu,kuna nyuzi IPPMEDIA yenye tittle ''Soo la EPA:Gavana Ndullu atajwa!"
sikuweza kuisoma,wenye access ya mtandao watugawie tafadhari.

Magazeti ya mchana mengi ni udaku ila nyuzi zaidi ni kesho ama taarifa ya habari kama hawataona soo kusema ukweli .Maana TBC loh
 
it's not as juicy as the headline sounds folks! ni statement ya slaa, the man hasn't been charged with anything,yet...
 
Soo la EPA: Gavana Ndullu atajwa!

2008-11-11 17:19:44
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Wakati watuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA, wanazidi kuongezeka, sakata hilo limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa madai mapya yanayomhusisha gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu.

Katika madai hayo, inaelezwa kuwa Profesa Ndullu aliyenyaka nafasi hiyo baada ya gavana aliyekuwepo, Dk. Daud Balali ambaye sasa ni marehemu kutimuliwa kazi, hakustahili kushikilia nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa Balali aliyeboronga hadi mapesa hayo yakabebwa kiulaini.

Aliyeibua madai hayo ni Mbunge wa jimbo la Karatu, Dk. Wilbroad Slaa.

``Binafsi nilishangaa kuona Prof. Ndullu akipandishwa cheo na kuwa gavana mpya... ikumbukwe kuwa mapendekezo ya kampuni iliyokagua na kubaini wizi huo wa pesa za EPA
( Ernst & Young), yalitaka safu nzima ya uongozi wa BoT ibadilishwe,`` akadai Dk. Slaa.

Akadai kuwa kwa vile Prof. Ndullu alikuwa miongoni mwa safu hiyo, hakupaswa kupewa ugavana.

Sambamba na hilo, Dk. Slaa amedai kuwa bado hajaridhishwa na watu walioburuzwa mahakamani kwa kile alichodai kuwa, anaamini wapo vigogo wanaostahili kuunganishwa na watuhumiwa hao katika kesi zinazowakabili.

Akadai kuwa kwa anavyoamini yeye, wafanyakazi wa BoT walioshitakiwa katika kesi hiyo hadi sasa, ni baadhi tu ya watuhumiwa wa sakata hilo, kwani vigogo wa kweli walioidhisha fedha hizo hadi zikaweza kuchotwa kwa kiwango kilichotajwa bado hawajaguswa.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amesema licha ya baadhi ya watumishi wa BoT kuburuzwa kortini, bado Serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina juu ya sababu za kutomhoji gavana wa awali, Dk. Daudi Balali kuhusiana na wizi huo wa EPA.

``Nadhani maelezo ya Ballali yalihitajika sana…yeye ndiye alikuwa na ufunguo wa mambo yote, hivyo Serikali iueleze umma ni kwa nini haikumhoji,`` akasisitiza Dk. Slaa.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, ametaka watu waliorudisha fedha za EPA nao wafikishwe mahakamani.

Akasema taaluma ya sheria aliyofundishwa na ile anayoendelea kuwafundisha wasomi wa Watanzania na pia katiba ya nchi, inaeleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

Akasema kwa mtaji huo, haoni sababu ya kuwaacha watuhumiwa waliorejesha fedha za EPA bila kuwaburuza kortini.

``Kutowafikisha mahakamani wale waliorudisha fedha ni ubaguzi wa wazi mbele ya sheria. Kwa vile mimi ni mwalimu wa sheria, sivumilii kuona hali hiyo,`` akasema Dk. Mvungi.

Hadi kufikia jana, watuhumiwa 20 wa kesi ya EPA walikuwa tayari wameshaburuzwa kortini na kusomewa mashtaka ya kuhusika na wizi wa pesa hizo za EPA kabla ya kutupwa rumande, huku wawili pekee wakipata dhamana ambao ni Davies Kamungu na Godfrey Mosha.

Miongoni mwa walioburuzwa kortini ni maafisa wanne wa Benki Kuu (BoT) ambao ni Mkuu wa Idara ya Madeni, Imani Mwakosya, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni , Esther Komu, Kaimu Mwanasheria, Bosco Kimela na Mwanasheria wa Benki hiyo, Sofia Joseph.

Wengine ambao wameshaburuzwa kortini na kutupwa rumande ni Jayantkumar Chandubhai Patel a.k.a Jeetu Patel, Devendra K. Vinodbhai Patel, Amit Nandy, Kehan Chohan na Johnson Lukaza, Eddah Mwakale, Manase Mwakale na Bahati Mahenge.

Waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni Mwesiga Lukaza, Jai Chohotalal Somani na Ajay Suryakant Somani.

SOURCE: Alasiri
 
Kuna mtu hapa alikurupuka kudai kwamba Lukaza ameshapata dhamana sasa mbona inaelekea bado anasota huko VIP ya Keko/Segerea?
 
Hadi kufikia jana, watuhumiwa 20 wa kesi ya EPA walikuwa tayari wameshaburuzwa kortini na kusomewa mashtaka ya kuhusika na wizi wa pesa hizo za EPA kabla ya kutupwa rumande, huku wawili pekee wakipata dhamana ambao ni Davies Kamungu na Godfrey Mosha.

Kuna mtu hapa alikurupuka kudai kwamba Lukaza ameshapata dhamana sasa mbona inaelekea bado anasota huko VIP ya Keko/Segerea?

Sawa sawa mkuu, tupo on the same page
 
Kichwa cha habari na ukisoma habari yenyewe vyote vimeniacha hoi utadhani mtu anaongea na msela(rafiki)wake kijiweni.
 
Kichwa cha habari na ukisoma habari yenyewe vyote vimeniacha hoi utadhani mtu anaongea na msela(rafiki)wake kijiweni.

Waandishi wabongo wengine wanakatisha tamaa na uandishi wao. Mimi ningekuwa mwenye gazeti waandishi kama hawa unawapa muda wa kuandika habari katika lugha fasaha na siyo za mitaani vinginevyo watapoteza kazi zao.
 
-TUKIWASHITAKI WOTE UCHUMI WA NCHI UTAYUMBA
Wanandugu maneno haya yamentisha si kidogo bali ni kwa hali ya tahadhar kwa kusikia maneno kama haya toka kwa mtu mkubwa kama huyu
kwamba mafisadi wameshika nchi hii so ni vigumu kuwafkisha wote !!!
JF NAOMBA TUSHAURIANE KWA HILI!!!!
kwangu mimi nahisi uchumi umeshayumba kama yeye binafsi hosea mshitakiwa na mshiriki halisi wa EPA ,bado ndie kinara namba moja kuchunguza fisadi wenzake!!!
pili ....tuwaachie wenyewe
 
Kwenye gazeti la mwananchi kichwa cha habari cha mbele ndugu yangu kikiwa na picha yake kubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Soma Gazeti la Mwananchi Toleo la Leo...

Ni KWELI Mafisadi WAMESHIKILIA UCHUMI na hilo halina ubishi Mr Impossible!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…