EPA na mambo yake

CHADEMA: CCM inahusika wizi wa EPA

na Edward Kinabo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kusisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinahusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alipohutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembe Togwa.

Alisema CCM inahusika na wizi wa fedha hizo, kwani chama hicho ndicho kilichotoa maelekezo kwa makampuni yanayotuhumiwa kuiba fedha hizo.

Alisema CCM ilitumia makampuni hewa yaliyoanzishwa kughushi na kujipatia fedha hizo kwa ajili ya kugharamia kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani kwa ushindi wa asimilia 80.

Akitoa mfano Zitto alisema, kutokana na rekodi za kibenki za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CHADEMA ilibaini CCM iliitumia kampuni hewa ya Deep Green Finance, kuchota sh bilioni 10.4, katika kipindi cha miezi minne kati ya Agosti mosi na Desemba 10 mwaka 2005, na kisha kampuni hiyo kutoweka katika faili la Msajili wa makampuni nchini (BRELA).

Alisema katika kipindi hicho CCM pia iliitumia Kampuni ya Tangold Ltd ambayo haikuwa imesajiliwa kisheria, kujichotea kiasi kingine cha sh bilioni 9 kwa madhumuni hayo hayo ya kugharamia kampeni zake.

Aidha, alisema baadhi ya viongozi wa CCM wana uhusiano wa moja kwa moja na Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ambayo ni moja ya kampuni kadhaa zinazodaiwa kuhusika na wizi huo, na kujipatia fedha kwa ajili ya kampeni, lakini vigogo wa CCM waliohusika na wizi huo hawajafikishwa mahakamani.

Alisema, CCM ilimtumia pia mfanyabiashara mmoja maarufu mwenye asili ya Kiasia (jina tunalo) kujipatia kiasi kingine cha fedha, na licha ya mfanyabiashara huyo kurejesha fedha alizochukua bado alifikishwa mahakamani kwa sababu ya kukataa kurejesha kiasi kingine cha fedha.

Alisema mfanyabiashara huyo aliikatalia serikali ya CCM, kurejesha sehemu ya fedha alizochukua kwa sababu kiasi hicho cha fedha ndicho alichokitumia kuwanunulia viongozi wa CCM magari aina ya Mahandra.

“Kama CCM inabisha kwamba haikufadhiliwa wala kununuliwa magari na mtuhumiwa huyo wa EPA, itoe vielelezo vyote vinavyothibitisha kwamba walinunua wenyewe magari hayo. Itoe risiti zote za usajili wa ....na iseme ilitumia fedha kiasi gani wakati wa kampeni. Iseme ilizipata wapi fedha hizo,” alisema Zitto huku akishangiliwa.

Alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, hajui chochote kuhusiana na jinsi chama chake kilivyopata fedha za kampeni ndiyo maana amekuwa akitetea.

Alisema Chiligati hajui kwa sababu kampeni za CCM wakati wa uchaguzi mkuu 2005, hazikuratibiwa na viongozi wa makao makuu ya chama hicho, bali ziliratibiwa na kundi maarufu la wanamtandao lililokuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Rais Kikwete, tangu katika hatua za awali za uteuzi wa mgombea wa chama hicho.

Alisema kwa mara ya kwanza, sakata la wizi wa fedha za EPA, liliibuliwa bungeni na Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa, lakini wabunge na viongozi wa CCM walisema Slaa alitumia nyaraka za kughushi na hoja yake ilikuwa ya uongo.

Aliendelea kufafanua kwamba, sakata hilo lilipozidi serikali ililazimika kutumia kampuni kufanya ukaguzi ambayo ilithibitisha kwamba ilikuwa ni kweli.

Alisema suluhisho la msingi la kushughulikia kwa haki watuhumiwa wote wa EPA na kuhakikisha kwamba wizi huo hautokei tena, ni kwa serikali kuanzisha Mahakama Maalumu ‘Tribunal’ itakayohusisha wanasheria na majaji wastaafu wanaoheshimika na kuaminika nchini pamoja na wataalamu wazoefu wa masuala ya fedha, kwa ajili ya kushughulikia tuhuma zote za EPA.

Alisema bilioni 133 zilizoibwa ni fedha za umma na wala wananchi wasikubali kudanganywa kwamba fedha hizo si za serikali.

Katika mkutano huo, aliyekuwa kada maarufu wa Chama cha Wananchi CUF katika manispaa hiyo, Mlaki Mdemu, alitangaza kujiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama na Zitto.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo, waliichangia CHADEMA, takriban sh 300,000 na kukitaka chama hicho kiende kwenye Jimbo la Mbeya Vijijini, ambalo liko wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Richard Nyaulawa, kilichotokea hivi karibuni.

Hata hivyo, Zitto aliwaambia wananchi hao kwamba CHADEMA inakusudia kusimamisha mgombea katika jimbo hilo, lakini kwa sasa haiwezi kufanya lolote, kwa kuwa bado inaomboleza msiba huo.

Tanzania Daima
 
misiamini kama Usalama wa Taifa wa nchi hii wamelala, iko hivi chochote kitachotakafanyika watakijua tuu ila utapigwa stop na majuto makubwa kama hiyo ishu ni yako au laa kama ni ya pesa nao natachangamkia deal, sasa usiniambie UWT kama UWT walikuwa hawajui ishu ya EPA.. na wasinge weza kuiba vile kama serikali haijui (achana na vile vidagaa vidogo vifanyakazi walivovipeleka mahakamani), au kutokuwa na mkono, CCM NAWAKHAKIKISHIA HIVI, KAMA SI LEO AU KESHO... HII ISHU MTAWAJIBIKA TUU... NIKO HAPA NAWAMBIA!!!!
 
Days are numbered, CCM jeuri yao soon or later itawatokea puani!
 
Hawana jeuri wameshaanza kuhaha... hivi kweli mtu na akili zako unaweza kusema migomo inafadhiliwa na wazungu????? zifuatazo ni dadalili za kuishiwa jeuri 'hakuna mtu ndani ya ccm atakae niweza zaidi ya JK'......'ndani ya ccm Mi mfungwa'.....
 
Huku mitaani kama kweli watu watapata hamasa ya kupiga kura basi naamini CCM ndo mwanzo na mwisho sasa hivi....!
Jamani huku hali ni mbaya mitaani kwa hiki chama cha mafisadi.
Hebu niambieni mpinzani gani yupo kwenye tuhuma za EPA wale wote si CCM wale?na wengine wengi bado wamewaficha kabatini lakini mwisho wao umewadia,.
 
Hilo ni MUHIMU sana, kila mtanzania akiwa na mwamko ni haya mambo na wakati wa uchaguzi wakaamua kutumia haki yao ya msingi kuwachagua viongozi wanaowapenda na kuwaamini, ya TARIME yatakuwa mengi sana!
 
Naipenda sana nchi yangu, lakini mambo ambayo CCM imetufanyia ni ya unyama kabisa na dawa yao, ni kutowapa kura 2010. Na serikali ya muungwana ni sawa na kichwa cha mwendawazimu
 
Naona hapakuwepo na mwanaccm kwenye mkutano huo....Kwasababu ni ngumu kuaasume kuwa walikuwepo halafu hawakujitoa.

Nadhani CHADEMA ndiyo chama mbadala kwasasa maana naona wanaminyana mbavu kiaina ndani ya upinzani...Kama wananchi walio wengi wanapendelea mabadiliko basi wanajuwa cha kufanya wakati wa kupiga kura.

Kwa wale walioko hapo bongo ndio wanajuwa reality ya wananchi mitaani na msimamo wao...Inavyoelekea hapo Iringa hakuna ccm kabisa hapo.
 
EPA: Kama vile mchezo wa kuigiza (Raiamwema)

Mwandishi Wetu Novemba 19, 2008

Baadhi ya watuhumiwa walalamika wanasiasa kuwatosa

WAKATI baadhi ya watuhumiwa wakiwa wamekwisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), mbinu chafu zilizotumika na vigogo katika kuchota mabilioni ya fedha katika akaunti hiyo sasa zimebainika.

Mbinu hizo ni pamoja na kughushi nyaraka mbalimbali na kutumia kivuli cha siasa katika kupitisha nyaraka husika bila kufanyika kwa uhakiki wa kina wa uhalali wa nyaraka hizo, kazi iliyofanyika kwa kasi iliyowashangaza hata wakaguzi wazalendo na wale wa kimataifa waliopitia hesabu za BoT.

Mfano wa dhahiri uliotolewa tokea mwanzo ni ule wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, ambayo ilithibishwa tokea mwanzo jinsi vigogo walivyoghushi nyaraka za kampuni 12 za kigeni kuweza kujichotea kiasi cha Sh bilioni 40.

Katika mchakato huo, Kagoda ilighushi nyaraka mbalimbali kuweza kujichotea kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh bilioni 40), ikiwa ni pamoja na nyaraka hizo kupitishwa na maofisa wa BoT bila kufanyiwa uhakiki.

Waliowasha moto wa wizi huo walikuwa ni wakaguzi wa kimataifa wa kampuni ya Deloitte & Touche, ambao walitimuliwa na serikali baada ya kutokea kutokuelewana katika ukaguzi wa akaunti hiyo ambayo sasa inazidi kuisakama Serikali.

Deloitte & Touche, ambayo ilipewa kazi ya kukagua akaunti za BoT, ilikumbana na utata mkubwa katika akaunti ya EPA namba 99915091 01, na hivyo kuwa kiashirio cha kwanza cha utata mkubwa katika akaunti hiyo.

Maelezo yaliyoibua utata huo yanaonyesha kwamba aliyekuwa Gavana wa BoT, Marehemu Dk. Daudi Ballali, alianza kujulishwa mapema kuhusiana na wizi huo akipewa mfano wa dhahiri jinsi Kagoda Agriculture Limited ilivyoghushi nyaraka.

Mfano uliotolewa kudhihirisha uhalifu huo ni jinsi ambavyo mikataba ya ununuzi wa madeni kwa kampuni 12 ilivyosainiwa katika kipindi kifupi cha kati ya Septemba 10, 2005 na Novemba 5, 2005, kipindi ambacho kilielezwa kuwa ni vigumu kwa wahusika kutembelea mbalimbali duniani kutiliana saini.

Aidha, imefahamika kwamba nyaraka zote zilisainiwa na wakili mmoja tu B.M. Sanze, na kati ya hizo mikataba minne ilisainiwa Oktoba 18, 2005 na mitano ilisainiwa siku moja baadaye Oktoba 19, 2005, jambo ambalo lilitia shaka jinsi wawakilishi wa kampuni hizo za kigeni walivyoweza kusafiri kwa wakati mmoja wakitofautiana kwa saa chache, jambo ambalo lilishindwa kuthibitishwa kwa kutumia kumbukumbu za Uhamiaji.

Katika nyaraka hizo, mikataba miwili iliyosainiwa Oktoba 18, 2005 kuhusiana na kampuni mbili za Ujerumani, Lindeteves J Export BV na Hoechst ikionyesha kwamba kulikuwa na deni la Euro 1,164,402.76 badala ya fedha za Ujerumani (Deutsche Marks.)

Wachunguzi na wakaguzi wameshitushwa na kasi ya ajabu ya jinsi marekebisho ya makosa hayo yalivyofanyika kwa kipindi kifupi baada ya BoT kuifahamisha Kagoda Agriculture Limited; huku barua ya kutaka marekebisho yafanyike ikiwa na maelekezo ya kuidhinisha malipo ya Sh 8,196,673,600.53 kwenda kwenye akaunti ya Kagoda. Kampuni hiyo iliwasilisha mkataba uliorekebishwa siku mbili tu baada ya kujulishwa.

"Haiwezekani hata kidogo kwa kampuni ya kigeni inayodai kuandika fedha zisizo sahihi huku BoT ikiendelea kuidhinisha malipo bila kuhakiki mikataba yote 12 ambayo imeonekana kufanana kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na maneno," inaeleza sehemu ya waraka wa wakaguzi.

Pamoja na kubainika kuwa mikataba na nyaraka zote hazikuwa na nembo ya kampuni huusika, nyaraka zote zilisainiwa katika ukurasa mmoja pekee wa mwisho tofauti na nyaraka za kisheria zinavyopasa kuwa.

Uchunguzi wa kina umebaini kufanana kwa mihuri ya kampuni zote zilizopitishwa ikiwa inalandana kabisa na muhuri wa kampuni za Kitanzania, tofauti ikiwa ni majina na anuani ya kampuni husika.

Mfano uliotolewa ni wa kampuni za Kitaliano za Fiat Veicoli Industriali na Adriano Gardella S.P.A pamoja na kampuni ya Kimarekani ya Valmet ambazo zote zimeonekana kuwa na mihuri na lugha zilizofanana katika nyaraka zote.

Utata mwingine uliodhihirika kughushi ni katika mkataba wa kampuni ya Valmet ya Marekani uliohusu Dola za Marekani 2,398,439.96 kusainiwa na Patrick Kevin, aliyetajwa kuwa Mhasibu wa kampuni hiyo, jambo ambalo limeelezwa kwamba ingekuwa vigumu kwa mhasibu kuachiwa kufanya kazi hiyo.

Utata mwingine uliobainika ni katika mkataba wa kampuni ya Daimler Benz AG ambao ulionyesha kusainiwa na Mkurugenzi aliyetajwa kwa jina la Christopher Williams, huku sahihi yake ikisomeka 'W Christopher'.

Uchunguzi wa ziada ulithibitisha kwamba baadhi ya kampuni zilikwishakufa wakati mikataba hiyo ikisainiwa na kampuni za Kitanzania, jambo ambalo linaendelea kuthibitisha wizi mkubwa wa kutumia maandishi uliofanywa katika akaunti ya EPA.

Mifano hai ni kampuni za Hoechst AG iliyobadilika na kuwa Aventis mwaka 1999, Daimler Benz AG iliyobadilika na kuwa Daimler Chrysler AG mwaka 1998 na Fiat Veicoli Industriali iliyobadilishwa na kuwa Industrial Vehicle Corporation (IVECO) tokea Januar1 1, 1975.

Kampuni nyingine zilizobadilika ni Mirrlees Blackstone kuwa MAN B&W Diesel Limited mwaka 2002/03 na Valmet iliyobadilishwa na kuwa Metso Paper kuanzia Mei 10, 2000. Utata huo uliwafanya wachunguzi na wakaguzi kujiuliza ilikuwaje kampuni zote hizo kuingia mikataba mwaka 2005 kwa kutumia majina ya zamani.

Pamoja na kuingiwa kwa mikataba hiyo na kampuni zilizokwisha badilishwa majina na umiliki wake, kampuni za sasa zenye uhusiano na kampuni zilizoingia mkataba zimekanusha kufahamu watu waliotajwa kuziwakilisha katika mikataba hiyo.

Kagoda ambayo ilisajiliwa Septemba 29, 2005, na kujichotea Sh bilioni 40 katika kipindi cha mwezi mmoja tu, jambo ambalo limewashangaza wengi kuona kampuni ngeni isiyofahamika inawezaje kuaminiwa kiasi kikubwa cha fedha bila kuhakikiwa.

"Inashangaza jinsi BoT ilivyoweza kuamini kampuni mpya kuwasilisha nyaraka za mabilioni ya fedha kwa kuingia makubaliano na kampuni za kigeni katika nchi za Ujerumani, Italia, Yugoslavia, Uingereza, Marekani na Japan kwa muda mfupi kiasi hicho bila kutilia shaka," wamehoji wakaguzi waliokagua hesabu za BoT.

Tayari kampuni ya Kagoda Agricultural Limited imekuwa gumzo katika sakata zima la EPA. Inafahamika kwamba kati ya shilingi bilioni 90 zilizoibwa katika akaunti ya EPA, sehemu kubwa ilichukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited ambayo hadi sasa wahusika wake hawajaguswa pamoja na kujitokeza kwa vigogo wawili kurejesha fedha zilizoibwa na kampuni hiyo.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba sehemu kubwa ya Shilingi bilioni 90 zilizothibitika kuchukuliwa kihalifu zilichukuliwa na makundi mawili tu, kundi la kwanza likiwa chini ya Jeetu Patel na lingine likiwa chini ya usimamizi wa vigogo wawili waliotumia kampuni ya Kagoda.

Imefahamika kwamba kwa sasa kuna hekaheka kubwa za kutaka kuzuia kushitakiwa kwa wahusika wa Kagoda, lakini vyanzo vya ndani ya Serikali vimeeleza kwamba kwa sasa Serikali haitabiriki na lolote linaweza kutokea wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka.

Kumekuwa na utata kuhusiana na ilipo na umiliki wa Kagoda Agricultural Limited. Hakuna anayeweza kubainisha hasa zilipo ofisi na wahusika wa kampuni hiyo tata.

Kumbukumbu za BRELA zinaonyesha kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina makampuni tofauti jirani lakini namba iliyotajwa haionekani na badala yake eneo lenye ofisi na kampuni viwanja vyenye namba 77, 86 na 88 katika eneo hilo la viwanda.

Katika ukaguzi wake wa awali wa mkaguzi wa nje Samuel Sithole kutoka kampuni ya Kimataifa ya Deloitte & Touche yenye makao yake Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo "nyeti" ya kiusalama.

Hata hivyo siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na aliyekua Gavana, Dk. Daudi Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo makini ambaye alijikuta akiachwa nje ya Baraza la Mawaziri.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema serikali yake haitomuingilia Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), watuhumiwa wengi walikamatwa na kufikishwa mahakamani walikuwa wamejiaminisha kuwa wamekwishapona na sasa waliobaki "hawalali" kuhofia kushitukizwa na kupandishwa kizimbani.

Tayari watu 20 wamekwisha kufikishwa mahakamani baada ya wafanyabiashara watatu kufikishwa mahakamani Jumatatu wiki hii wakitanguliwa na watuhumiwa wengine wakiwamo watumishi wa BoT waliohusika katika mchakato wa wizi huo.

Waliopandishwa kizimbani ni Ajay Somani na Jai Somani wanaodaiwa kula njama ya wizi wakiwa na watu wengine ambao hawajafahamika kuiibia BoT na kwamba Septemba 2, 2005 waliiba Sh. bilioni 5.9 mali ya benki hiyo.

Mtuhumiwa mwingine aliyefikishwa mahamani ni mfanyabiashara Mwesiga Lukaza, aliyepandishwa kizimbani akiunganishwa na mshtakiwa mwingine Johnson Lukaza, ambaye alishapandishwa kizimbani mapema wiki hii.

Watuhumiwa wengine ambao tayari wamefikishwa mahakamani ni Farijala Hussein, Rajab Maranda, Japhet Lema, Bahati Mahenge, Davis Kamungu, Godfrey Mosha, Manase Mwakale na Eddah Mwakale, Devendra Vinodbhai Patel, Amit Nandy, Ketan Chohan, Jayantkumar Chandubahi Patel na Johnson Lukaza.

Wengine ni wafanyakazi wa BoT ambao ni Mkuu wa Idara ya Madeni ya Biashara, Iman David Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni, Ester Mary Komu na makaimu Katibu wa benki wawili ambao ni Bosco Ndimbo Kimela na Sofia Joseph Lakila
 
Tusidanganyane, lofa hawezi kuchangiwa milioni 104.
 
Au nilisikia vibaya? Huyu Ester Mary Komu ana uhusiano gani na Grace Kiwelu, mbunge wa CHADEMA? Wakati anatoka mahakamani - jana nafikiri, aliingia kwenye gari la Grace. ITV walielezea habari hii, ikiambatana na video footage.

.
 
EPA: Kama vile mchezo wa kuigiza

Mwandishi Wetu Novemba 19, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Wengine ni wafanyakazi wa BoT ambao ni Mkuu wa Idara ya Madeni ya Biashara, Iman David Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni, Ester Mary Komu na makaimu Katibu wa benki wawili ambao ni Bosco Ndimbo Kimela na Sofia Joseph Lakila.
 
kwa wastani wa laki laki, then ni watu 1040 waliomchangia, sasa ukiirekebisha hiyo hesabu, kwa kuwa umesema watu wengine walitoa elfu kumi kumi, unaweza kukuta watu kama elfu mbili mpaka tatu au hata zaidi walimchangia.
 
IGP aonya hakuna kigogo EPA atapona
*ASEMA NI SUAIGP aonya hakuna kigogo EPA atapona
*ASEMA NI SUALA LA WAKATI, AONYA WANAFUNZI

Na Ummy Muya

WAKATI baadhi ya watu wakihoji ukimya wa kutofikishwa kwa baadhi ya watuhumiwa vigogo waliochota fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema, amesema hakuna wa kupona EPA na kwamba, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.

Kauli ya IGP Mwema ni ya tatu kutolewa na wajumbe wa Timu ya Rais ya EPA, kwani tayari Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliazer Feleshi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Edward Hosea, wameonya kwamba hakuna mtu aliyehusika na tuhuma hizo atakayepona.

Akijibu swali Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dares Salaam jana kuhusu kwa nini hadi sasa vigogo wa EPA hawajakamtwa na ni lini watafikishwa mahakamani, IGP Mwema, alisema wale wote waliojichotea fedha za akaunti hiyo wako njiani kufikishwa mahakamani.

"Vigogo ni wakina nani? Kesi inaendelea na wanaofikishwa mahakamani ni wale ambao taratibu muhimu zinazohitajika zimekamilika na wengine watafikishwa mahakamani, taratibu zikikamilika," alisema.

Kusisitiza kauli yake, Mwema alisema hakuna mtu atakayeonewa na kwamba, mchakato huo si kiini macho kwani wahusika wote watafikishwa katika vyombo vya sheria kwa mujibu wa katiba, zitafuata mkondo wake.

IGP akizungumzia mchakato huo mzima na kitisho kutoka kwa baadhi ya watuhumiwa wa EPA kwa mahakimu wa Kisutu, alikiri kuwepo kwa hali hiyo kwani tayari malalamiko yamefika katika ofisi yake.

Alisema malalamiko ya mahakimu hao yanatokana na kile walichokiita kwamba, ni kutishiwa usalama wao kutokana na kazi zao katika uendeshaji wa kesi za EPA.

"Sisi jeshi la polisi tuko pamoja nao na kuhakikisha hawapati madhara kutokana na vitisho hivyo wawapo kazini na sehemu nyingine,"alisisitiza Mwema.

Alisema kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi hairuhusu mtu, watu, ama kikundi kuvuruga amani kwa makusudi kwa maslahi yao binafsi.

Kuhusu migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambayo ilikuwa ni moja ya jambo aliloitishia mkutano na waandishi wa habari, alikiri kwamba inatishia amani na utulivu.

Alisema suala la amani na utulivu nchini ni muhimu, hivyo jeshi lake limeamua kufanya uchunguzi kufuatia malalamiko ya wanafunzi ya kupigwa na kufanyiwa fujo katika migomo inayoendelea.

"Tunasisitiza kwamba, demokrasia ipo na iendelee kuwepo, lakini iende sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu," alionya.

Alisema si kweli kukuwa kwa demokrasia kunaruhusu kuwepo kwa vurugu na upotevu wa amani, hivyo jeshi la polisi nchini halitafumbia macho vitendo hivyo viovu na kuhatarisha usalama wa nchi kwa madai ya kukuwa kwa demokrasia.

"Uchunguzi kamili umeanza sambamba na kupata maelezo mbali mbali kutoka kwa viongozi mbalimbali katika vyuo husika ili kubaini ukweli," alisema.

Viongozi ambao tayari wameshazungumza nao ni viongozi wa chuo cha Ardhi, Mlimani, Mkwawa, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Duce), na Chuo cha Kilimo Morogoro (Sua) na kuwaachia isipokuwa Julius Mutatilo, ambaye alifikishwa mahakamani.

Alisema wanamshikilia mwanafunzi mmoja raia wa Uganda Odoli, ambaye wanaendelea kumhoji kutokana na kuhusishwa na vitendo vya ushawishi kama historia yake inavyojionyesha.

Kwa msisitizo, alisema jeshi hilo liko karibu na viongozi wa wanafunzi na kutaka kupewa taarifa kama kuna wanaochochea migomo hiyo ya wanafunzi wa vyuo nchini.

Suala la EPA na migomo ya wanafunzi ni mambo ambayo hadi sasa yanaitikisa nchi, kufuatia kuwepo na mvutano kutoka kwa wadau mbalimbali, serikali na vyombo vya dola.

Wakati watu wakitaka vigogo zaidi wa EPA wakamatwe na kufikishwa mahakamani, hadi sasa bado kuna ukimya huku kwa upande wa migomo ya vyuo vikuu serikali ikiamua kuvifunga na vyombo vya dola kukamata baadhi ya wanafunzi kwa tuhuma za uchochezi.

LA LA WAKATI, AONYA WANAFUNZI

Huyu kweli mwendawazimu mwenzake dpp ameshasema yeye ndie
mwisho wa matatizo !!!hakuna zaidi yake na hatokaa akae kutafuta mmiliki
wa kampuni ya kigoda !!kama si kufanya wapumbavu nini??epa bila kagoda ni sawa na rais kikwete bila mama salma!!tena nashauri aache kuendelea kutangaza utmbo kama kumwona tushachoka kumuangalia kwenye tv

aanze na kigoda na meremeta ziko wapi ,wamiliki ni nani wanafiki wakubwa
mungu uwashugulikie wanafiki wote hao wakiongozwa na rais wao kikwete
kwa kukaa na wakina lukaza na jeetu kuwashauri wakubali kukamatwa na kutoka kwa mdhamana ili waume zao((imf na wengineo_)waweze toa misaada

dem

tanzania inanuka na itaendelea kunuka
 
kwi kwi kwi kwi kwi...... mama mia ni KAGODA si KIGODA bana
 
‘Kada wa CCM alikiri kuchota mamilioni BoT’

Shadrack Sagati na Neema Mgonja
Daily News; Thursday,November 20, 2008 @21:15

Kigoma Mjini wanajua vyema kuwa jamaa ni mwizi na ni pesa zake ambazo Makamba alizutumia 'kuua' Tawi la CHADEMA la Urusi na matokeo yake vijana 3 tu wakagawana na kisha Magazeti yakatangaza kuwa Ngome ya CHADEMA Kigoma imefungwa na kuwa ya CCM!

2010 CCM Kigoma Mjini wna kazi kubwa sana kutetea hilo Jimbo sbabu moja wapo ni huyo Fisadi Maranda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…