EPA na mambo yake

Baadhi ya Wezi EPA wamepelekwa mahakama ya Kisutu Leo ,kuna msg ilikuwa inapitishwa kwenye TV -Chanel Ten ,there was no further info ,i was watching Obama's Victory Speech .
 

Ndugu yangu Bubu
Nilimwambia ndugu yangu Halisi kuwa hii haikuwa breaking news maana hakuwa na data kamili, hadi sasa hajafanikiwa kuweka hizi data hapa. Kuna uwezekano kasikia kuwa kuna watu wamepelekwa Mahakamani! Ni nani na nani? Hajatwambia. Aweke hizi data hapa Jamvini watu wajue kwa kina!
 
ni kuhusu mafisadi walishindwa kurudisha pesa za EPA.nasikia wamekamatwa mmoja wao anaitwa D.Ka........
kama kuna zaidi leteni
 
Jamani any new updates on the matter?nani kakamatwa mpaka sasa?
 
ni kuhusu mafisadi walishindwa kurudisha pesa za EPA.nasikia wamekamatwa mmoja wao anaitwa D.Ka........
kama kuna zaidi leteni

Vica kama unalijua hilo jina si uliweke tuu watu walichambue? D.Ka ndio nani?
 
Wajameni twendeni taratibu hapa katika epa,kwani kuna watu muhimu tutawasahau,ambao ni muhimu,cadre ya kina mgonja na meghj
 

....well....not from Halisi....BAK umemsahau Halisi!!!........
 
Kama Jetu Patel kakamatwa kweli basi huu ni uwongo wa hali ya juu. Hii serikali ya JK inawakumbatia wezi wa EPA na vipi serikali hiyohiyo iwakamate wezi wa EPA?Au JK kabadilika?
 
ni kuhusu mafisadi walishindwa kurudisha pesa za EPA.nasikia wamekamatwa mmoja wao anaitwa D.Ka........
kama kuna zaidi leteni
...Inakuwaje sasa mbona unatoa habari vipande vipande??? D.Ka......ndio nini si useme tu???Ah!!??
 
Jeetu Patel kakamatwa na alikuwa afikishwe Mahakama ya Kisutu leo..

Ameshafikishwa na watu wengine kadhaa wakiwamo baadhi kutoka katika familia yake na mtu mmoja anaitwa Lukanza au Lukaza. Wanakabiliwa na kesi mbili ambazo kwa ujumla mashitaka yake ni wizi na kughushi.
Hakimu amewapeleka rumande wakapumzike akisema kuwa muda wa kutoa uamuzi kuhusu dhamana ulikuwa umekwisha. Hivyo kesho watarudishwa tena mahakamani kwa ajili ya kuja kusikiliza iwapo watapata dhamana au la
 
Mmh ila habari za kusikia nazo, tunashindwa hata kuzitetea...Mimi nimesikia kuwa wapo waliopo Kisutu kwa shughuli ya EPA, lakini ni wale 'kondoo wa sadaka' tu...
 
Baadhi ya picha za watuhumiwa wakiwa mahakamani ziko....

Hizi hapa:


Kutoka kushoto Lavendra Vinod Bhai, Amith Nandi na Jant Kumar wakiwa mahakama ya kisutu mchana huu. Wanatuhumiwa kuchota bilioni 10 kila mmoja.

..hawa nao wamo, kushoto ni Bw. Johnson Mutachukurwa Rwekaza anayedaiwa kuchota bilioni 6.3. Wengine majina yao hayakuweza kujulikana mara moja! Wameshindwa masharti ya dhamana na wametupwa lupango hadi Novemba 18 kesi yao itakapotajwa tena! habari ndiyo hiyo!!!
 
Mmh ila habari za kusikia nazo, tunashindwa hata kuzitetea...Mimi nimesikia kuwa wapo waliopo Kisutu kwa shughuli ya EPA, lakini ni wale 'kondoo wa sadaka' tu...

Hapa kila mtu na lake.... Kama kitu hujui nyamaza usisema habari za kusikia. Wanasema hata kila Lukaza wamo ila Maregesi ndio hayumo. Yuko mwanasheria anaitwa Kamala wa Professional Law
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 163 (54 members and 109 guests)

Ahsante Kigoma..... JF oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Tunapeta kama Obama...................

sasa cheers!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1 Glass
 
Haya jamani! Habari ndio hiyo. Hayawi hayawi, ndio kama yanakuwa vile. Ngoja tuone mwisho wake.
 

hii ni sanaa tupu...maana hawa ni wale walioshindwa kurudisha. waliorudisha wako wapi? we want big names here
 

sasa mbona Jeetu Patel haonekani kwenye picha???
au mpiga picha ndiye kamsahau???kwa maana Jeetu ndiye muhimu zaidi kuliko wote,kwa kutilia maanani habari ambazo zimekuwa zikisemwa kuwa serikali imekiri kuwa hakamatiki mara yuko nje ya nchi.Na mwanzo wa thread hii imeripotiwa kuwa naye amekamatwa na kufukishwa kisutu,jamani mimi bado sina amini kama mtuhumiwa namba moja Jeetu Patel amekamatwa,labda nione picha yake hapo angalau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…