EPL: Chelsea, Spurs zatoka sare ya 2-2, Harry Kane apiga bao dakika ya 90+

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Goli la dakika 90 mfungaji akiwa ni Harry Kane wa Tottenham limekatisha furaha ya Chelsea ambapo limesababisha mechi baina ya timu hizo kumalizika kwa sare ya 2-2 katika Premier League, leo Agosti 14, 2022 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Kalidou Koulibaly na Reece James ndio waliofunga magoli ya Chelsea wakati lile la kwanza la Tottenham likifungwa na Pierre-Emile Hojbjerg.

Aidha, katika mchezo huo makocha wa timu hizo, Antonio Conte wa Chelsea na Thomas Tuchel walipewa onyo na mwamuzi kutokana na kurushiana maneno wakati mchezo ukiendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…