Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Ligi kuu soka England kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa kwanza utapigwa saa 3 usiku ukiikutanisha Burley dhidi ya Fulham katika Dimba la Turf Moor.
Baada ya kuiadhibu Crystal palace bao 3-0 weekend iliyopita Burnley anakuja kukutana na Fulham ambaye naye alimtandika Everton bao 2-0.
Mchezo mwingine ni kati ya Everton ambaye atakuwa nyumbani kuialika Manchester city katika Dimba la Goodson park.
Manchester City watatafuta ushindi kwa nguvu ili kukamilisha alama 10 mbele ya anaewafuatia huku wakiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.
Vijana hao wa Pep Guardiola wana alama saba mbele ya anaewafuatia ambaye ni Manchester United wakiwa na mchezo mkononi, na wameweka rekodi ya kushinda mechi 16 katika mashindano yote.
Calro Ancelotti atakuwa na hamu kubwa ya kumrejesha mfungaji wake bora Calvert-Lewin mapema iwezekanavyo baada ya kuchezea kichapo cha goli 2-0 mbele ya Fulham juma lililopita.
Mechi hiyo iliwafanya washindwe kufunga kwa mara ya tatu mfululizo katika michezo minne ya Ligi hiyo wakiwa nyumbani huku wakifunga mara moja tu.
Hii haileti matumaini kwao ya kuweza kupambana na City, ambayo uimara wa safu yake ya ulinzi umeifanya kuwa na clean sheets 11 na kushinda michezo 16 wakiruhusu mabao matano tu .